Jumanne, 2 Desemba 2014

LOVE STORY

SIMULIZI: MY DIARY(KITABU CHA KUMBUKUMBU ZANGU)
SEHEMU YA 1
MTUNZI:ELIAS ADOLF(eliado)
FB PAGE: Eliado Love Stories
ANGALIZO: ISOMWE NA WATU WENYE UMRI KUANZIA MIAKA 18+

 
 Nilikuwa juu ya jukwaaa nikifanya vitu vyangu ili hali nikijua kabisa watu wote waliokuwa wakinitizama walikuwa wanaumia roho kutokana na mvuto wa umbo langu niliokuwa nao. Nilisikia mijibaba miwili ikiulizana hivi lile wowoo ni la kwake au ni la mchina? Mmoja wao akaropoka “wee kitu original hicho, kwani umemsaahau huyu binti tulishakutana nae kule Arusha mpaka tukambatiza jina la soda kubwa tena ya fanta yaani BAMBUCHA.?” Yeah nimekumbuka alidakia mwanaume wa tatu waliokuwa nao.

Akaongeza basi huyu tusimwite tena BAMBUCHA bali tumpe jina la bia kwani inaonesha thamani yake ni kubwa zaidi. Basi wote kwa pamoja wakacheka. Wakati nikiendelea kutingisha makalio yangu ambayo kiukweli yalikuwa yakitetemeka kama mawimbi ya bahari, Yule aliyetoa hoja akapendekeza jina linalofanana na bia eti kutokana na uzuri niliokuwa nao aliniita HAINKEN WOWOWO.

Ilinibidi nicheke kwa nguvu kitu ambacho kiliwashitua mashabiki wangu waliokuwa wakinifuatilia, hawakujua nilikuwa nikicheka nini wakajua labda nilifurahishwa na ule wimbo wa kanga ndembendembe laki si pesa. Wakati nikiendelea kuzungusha nyonga yangu kwa ufundi wa ajabu niliokuwa nao niliendelea kufuatilia mazunguzo ya wale watu waliokuwa wamekaa meza ya karibu na jukwaa. Niliendelea kuzungusha nyonga na kwa wale ambao ndo ilikuwa ni mara yao ya kwanza kuniona walishangaa sana.

Lakini kwa wale ambao walishaniona kwenye shindano la miss nyonga kule Arusha wasingeshangaa sana kwani kile ndo kipaji nilichojaliwa na mwenyezi Mungu.Nilizungusha kisawa sawa huku nikirembua macho yangu kitu ambacho siku zote kilikuwa nikiwaumiza wanaume wenye tamaa. Kwa ufundi wa ajabu nilio kuwa nao niliendelea kufuatilia wimbo niliowekewa huku nikilitegeza sikio langu moja kwenye ile meza iliyokuwa karibu yangu. Wale wanaume waliendelea kunitumbulia macho huku wakiendelea kubishana juu ya jina gani wangenibatiza kulingana na uzuri wangu.

Nilibahatika kumsikia mmoja akimwita muhudumu kwa fujo na kumwambia “inaelekea wewe hujui majukumu yako, mbona bia imeisha na umekaa mbali? Dada kwa heshima kubwa na kutambua kuwa walikuwa wameanza kulewa alimjibu kwa kumbaia samahani kaka” Sitaki samhani yako niletee bia inayofanana na huyo dada kwenye jukwaa. Yule muhudumu alibaki ameduwaa asijue nini cha kufanya. Akauliza jamani kaka mbona sikuelewi nikuletee kinywaji gani? Kaka kwa ukali akamwambia kinachofanana na huyo dada.

Muhudumu akaenda kaunta na alipokuja alikuja na soda kubwa iliyojazia yaani BAMBUCHA. Watu wote kwenye meza yao walishangaa yaani mtu alikuwa anakunywa bia na sasa ameletewa Bambucha. Ili bidi wapigwe na butwaa, yule jamaa akamuuliza yule muhudumu kwanini umeleta hii soda? Muhudumu kwa kujiamini alisema ‘Ni kwa sababu huyo dada anaitwa BAMBUCHA.Basi watu wote pale mezani waliangua kicheko.

Basi kwa kuwa kila mtu alipewa nyimbo tatu kuonesha maujuzi ya kuzungusha nyonga na kuchezesha makalio, hivyo mimi niliwekewa wimbo wangu wa mwisho. Huku nikibadilisha staili na kucheza ile matata ya kulala chini kisha kuzungusha kama vile upo juu ya mwanaume. Nilimsikia yule mteja akimwambia muhudumu niletee HAINKEN WOWOWO na wakati Yule dada akitafakari Heinken wowowo ni ipi, kwa macho yangu ya wizi nilimwona yule kaka akifungua pochi yake na kutoa hela na kila kwenye noti ya elfu kumi alikuwa akiandika kitu.

Sikujua alikuwa akiaandika nini nitakwambia nikishuka jukwaani. Basi nikaamua kuendelea kufanya yangu na nilikuwa namalizia na ile staili ya mdembwedo. Hii staili ni mbaya sana kwani unakuwa kama unajizalilisha, hapa wapambe wangu walinimwagia maji kwenye makalio hivyo kuwa ndembendembe. Nilitumia vizuri vidole vyangu kuviingiza sehemu ambazo kwa kweli naogopa kusema. Yule kaka akashindwa kuvumilia akanifuta na kunimwagia zile noti za elfu kumi kumi.

Sikujua alinipa shiling ngapi kwa kuwa haikuwa kazi yangu kuokota hela ila kwa utundu wangu niliivuta moja kwa kutumia vidole vya miguu yangu. Nilifanya hivyo kwa sababu mara nyingine huwa tunazulumiwa na pia nilitaka kujua yule kaka aliandika nini kwenye zile hela. Wakati nashuka ili kuruhusu mshiriki mwingine apande na kuendelea na vitu vyake, nilimsikia tena yule kaka akibishana na yule muhudumu “nimekwambia Heinken wowoo sio Mutungi.

Hapo nikajua yule kaka atakuwa amekaa sana nje ya nchi maaana zile bia watanzania wengi hawazinywi kwa kuhofia bei. Basi muhudumu alimwita meneja wa bar kwani ilionekana walikuwa hawaelewani. Basi meneja aliweza kumwelewa na kumpa bia iliyofanana na mimi.

Baadaye nilipewa zile hela zangu japo nilihisi wamenichakachua.Kumbe kwenye zile noti aliandika namba zake na mara baada ya shindano kuisha na mimi kutangazwa mshindi niliamua kumtafuta yule kaka. Aliongea mengi ila kubwa na la muhimu kwake eti alitangaza nia ya kunioa. Nilishangaa sana itawezekanaje umwone msichana siku moja umpende na utake kumwoa. Kwa kweli haikuniingia akilini na pia nilimwonea huruma sana kwa kuwa hakujua historia yangu.

Baadaye tulielewana na kwenda kuchukua chumba na kulala. Ingawa alinilipa hela yangu lakini hakutka tufanye mapenzi kitu ambacho sikuamini maishani mwangu kuwa mwanaume anaweza kulala na mwanamke mzuri kama mimi na hasifanye kitu chochote. Ilibidi niwe mkali lakini aliniambia anilipe mara mbili ili niwe nae kwani alikuwa anataka kujua hisoria yangu ya maisha.

Nikahisi labla alikuwa akifanya utafiti, basi nilimwambia historia yangu ni ndefu sana ingawa nimeeiandika kwenye diary yangu kwa leo siwezi kukupata hata robo labda kama tusilale.. Yule kaka aliendelea kunishangaaa. Nikamwambia atoe historia yake alafu ya kwangu nitamtafuta yule mwandishi mashuhuri Eliado aiandike kwenye kitabu.

Basi ingawa nilkuwa namjua kuwa ni star wa bongo movies, nilijifanya sijui chochote. Alieleza stori ndefu sana ya maisha yake hasa upande wa mahusiano na mafanikio yake. Nilimsikiliza sana na kwa kweli nilitokewa kuvutiwa nae japo kiukweli sikuwahi kufikiria kuwa nitakuja kuolewa maishani mangu hivyo ombi lake la kutaka kunioa liliniumiza sana hasa kutokana na ugumu wa historai yangu.

Baadaye alinimba niombe kushiriki shindano la big brother Africa na akasema kutokana na umaarufu wake atanipigania nipate nafasi hiyo. Nilifurahi sana maana siku zote niliamini nitakuja kuwa super star mkubwa sana wa nchi hii.Alisistiza kwamba pamoja na mambo mengine uzuri wangu ni kigezo tosha cha kucheza filamu hivyo ataniingiza kwenye filamu mpya ambayo ingetoka mwezi ujao.

Watanzania hawakuamini kuwa naweza kuwawakilisha vyema kwenye shindano la big brother Africa mpaka pale nilipotangazwa mshindi. Vyombo vya habari vya Tanzania na Afrika kwa ujumla vinmenizunguka wakitaka kujua historia yangu, napatwa na kigugumizi kwa kuwa historia yangu ni ngumu sana. Wazo la haraka ni kumpigia Elias Adolf maarufu kama eliado mwandishi mashuhuri aje kunisaidia maana mara ya mwisho alinambia ataniandalia kitabu cha kumbukumbu za maisha yangu****************************************

Nilikuwa hata sijajitambulisha kwani nilitaka mjue asili ya majina yangu maana kiukweli nilikuwa na majina mengi kabla na baada ya kuwa superstar. Ila nitatumia jina langu la asili nililopewa na wazazi wangu. Nilipozaliwa tu wazazi wangu waliniita Leah. Ni mtoto wa kimbulu niliyechanganya damu na mama wa kiharabu.Nina historia ndefu sana ambayo kiukweli inahuzunisha sana. 

Lakini kwa kuwa dunia mapito nitaeleza kwa kifupi hasa upande wa mahusianao na mapenzi. Mimi ni mtoto wa pekee wa kike katika familia ya mzee Bura mzee ambaye alikuwa ni maarufu na tajiri mkubwa pale jijini Arusha.

Ingawa nina mapungufu yangu ya kimaisha lakini kiukweli nimejaliwa uzuri ambao kwa namna moja au nyingine ndo chanzo cha kuharibikiwa na kisha kufanikiwa katika maisha yangu.Ni mweupe kiasi, mwenye umbo la kibantu na nyuma nimefungashia kama mlima kitonga. Nina sura ya mduara kama watoto wa kiharabu ambapo kwa haraka haraka ukikutana na mimi huwezi amini kuwa ni mtanzania tena wa Arusha. 

Mungu kanijalia umbo,sura, mwendo, macho na kila kiungo unachojua wewe kinaweza mvutia mwnaume.Ni mnene lakini si ule wa kuboa ni ule wa mpangilio na kwa kweli sina matiti makubwa. Nina macho ya mlegezo ambapo kiukweli nikikuangalia mara mbili ni lazima tu utanitamani. Kasoro yangu kubwa au kilema mungu alichonipa ni..................ITAENDELEA KESSHO.

Jumanne, 4 Novemba 2014

UHUSIANO



JINSI YA KUFANYA ILI KURUDIANA NA MPENZI WAKO WA ZAMANI-3

Leo tunaendelea na hatua ya 4 na ya mwisho katika muendelezo wa njia au jinsi ya kufanya kurudiana na mpenzi wako wa zamani. Kupata hatua za mwanzo bofya http://eliasadolf.blogspot.com au kwenye facebook page inayoitwa eliado love stories.
HATUA YA 4: WASILIANA NAE.
Kumbukuka mpenzi wako alipokuacha, alikuona na kukuchukulia wewe ni mkosaji, mdhaifu na usiyejiheshimu. Lakini kwa kitendo chako cha kumtomtafuta kwa mda, lazima ashangae na kujiuliza maswali mengi juu yako. Je, amepata mwingine mzuri zaidi yangu? Je hanipendi tena?........ 
Hapa ataanza kusahau madhaifu yako yote na kuanza kukukumbuka vitu vizuri ambavyo ulikuwa ukimfanyia. Ataanza kukumbuka vitu vizuri ulivyo navyo wewe. Pindi utakapowasiliana nae, hakikisha unaongea nae na ikibidi mnaonana. Vifuatavyo ni vitu vya kuzingatia kabla ujawasiliana nae.

  1. Umehakikisha hujawasiliana nae zaidi ya mwezi  
  2. Umefanya mabadiliko katika maisha yako
  3. Una uhakika kuwa kurudiana nae ni uamuzi sahihi 
  4. Umekubaliana na sababu za nyie kuachana
  5. Una uhakika kuwa hata kama hatokubali kurudiana na wewe utaendelea na maisha yako ya furaha.
NJIA ZA KUWASILIANA NAE
(a)    Barua pepe
Kwa kuwa barua imepitwa na wakati katika kizazi hichi cha digital, unaweza kutumia barua pepe au mitandao mingine ya kijamii. Barua pepe lazima iwe na malengo matatu
  1. Kumfanya mpenzi wako aolewe kuwa umekubaliana na hali ya wewe na yeye kuachana. Na kwamba pia haikuwa kitu kibaya
  2.   Kuomba msamaha sehemu zote ulizokosea
  3.   Kumjulisha kuwa kuna mambo mazuri yanaendelea kukutokea katika maisha yako, mfano kupata kazi, kununua gari. Ila usimweleze sana ili awe na hamu ya kujua zaidi nini kimetokea kwenye maisha yako mara baada ya kuachana.
(     (b)   Ujumbe mfupi wa maneno
Sms itume  mara baada ya kutuma barua pepe. Pia unaweza usitume barua ukatuma sms moja kwa moja, kwa sababu wewe ndo unamjua zaidi mpenzi wako tumia njia yoyote ambayo utakayoona ni sahihi au zote kwa pamoja.
Kitu cha kuzingatia hapa unapowasiliana nae usizungumzie moja kwa moja kuhusu uhusiano wenu. Pia epuka kutuma ujumbe usiojitosheleza. Ujumbe ambao utapunguza yeye kujibu kitu kwa mfano
“mambo” “i miss you” “upo” na zingine na kifupifupi.
Kamwe usizungumzie kuhusu hisia na mapenzi au unataka kurudiana nae kwa mfano
“ i love you” “nateseka sana juu ya penzi lako” i want you back na zingine unazozijua.
Epuka kusema kitu kibaya kwenye meseji kama “ watoto wako wanakukumbuka sana, ulifanya makosa sana kuwaacha wateseke” au “ kama usingekuwa na tamaa, naamini tusingeachana”
Ila unaweza kuandika vitu vifuatavyo katika ujumbe wako wa mneno
“ leo naangali filamu mpya ya Dimond na Wema, imenikumbusha pindi tukiwa pamoja.
Mkumbushe vitu ambavyo mlishawahi kufanya pindi mlipokuwa pamoja kwa mfano
“ Dah, nimekumbuka siku tulivyokwenda Marangu waterfalls, siku ile ilikuwa ya furaha sana. Nafurahi tulifurahia”au “Mambo, leo nimepika wali samaki nimekumbuka jinsi ulivyokuwa ukinipikia”.
MUOMBE MUONANE
Baada ya kuwasiliana nae muome muonane ana kwa ana, ila usimwambie kuwa ni siku ya kufanya mapenzi, bali ni siku ya kuonana tu. Usimwoneshe kuwa unataka kurudiana nae. Onesha kuwa unataka mtoke kama marafiki tu lakini unaweza kufanya vitu vya kumvutia mnapokuwa pamoja. 
Mfano kumkumbatia. Njia nzuri hapa ni kumkaribisha chakuala au kuenda naekuanagalia sinema au sehemu yoyote yenye burudani.
Baada ya hapo siku ingine lazinma takutafuta na kukuomaba muonane hapo usifanye makosa na kuzungumzia mambo mabaya yaliyowafanya muachane, zaidi tazama mbele anza upya. 
Siku hii ni nzuri kama mtalimenya tunda na kukumbushia enzi zenu. Amini sasa ni wako mpende kama zamani na sahau yaliyopiata wazungu wanasema “there is no point digging old graves when you want  to start a new life”....
KWA LEO TIUSHIE HAPA, ILA USIKOSE TOLEO LIJALO LINALOHUSU VITU VYA KUFANYA ILI USIACHANE NA MPENZI WAKO.

Jumatatu, 3 Novemba 2014

DARASA HURU



ZIFAHAMU FAIDA NA HASARA ZA KAHAWA NA CHAI.
Watu wengi wamekuwa wakibishana  kipi bora kunywa kati ya kahawa na chai? Watumiaji wa vinywaji hivi kila mmoja amekuwa akieleza umuhimu wa kinywaji anachokipenda. Lakini kiukweli vyote kwa pamoja vina faida na hasara. Vinywaji hivi viwili vyote vinaweza kuongeza vitamini na kusaidia ubongo. 

Pamoja na faida nyingi za vinywaji hivi lakini wanywaji wanashauriwa kunywa kwa kiasi kwa sababu vyote vina Coffeine anaonya DR Jane Scearce. Ni dhairi kuwa kuna mgongano wa fikra juu ya faida na hasara za vinywaji mbalimbali. Zipo tafiti zinazosema Kahawa na chai zina faida na wapo wanaosema zina hasara.
ZIFUATAZO NI FAIDA ZA CHAI.
Kuna aina nyingi za chai ambazo ushawahi kuzisikia baadhi yake ni nzuri na baadhi yake ni mbaya. Ufati unaonesha kuwa aina yoyote ya chai inaongeza na kusaidia kufanya kazi kwa homoni inayoitwa Insulini mara kumi na tano zaidi.
Chai ya kijani inaaminika kuwa na kitu kinachoitwa kitaalam Antiozidants ambacho ni muhimu katika kuzuia saratani ya matiti, mapafu na tumbo. Pia chai ya kijani inasaidia kuzuia kuzuia magonjwa yanayoshambulia moyo na kupunguza uwezekano wa kupata presha. Wataalam pia wanaeleza kuwa chai ya kijani pia inasidia kuunguza fati na kuyeyusha mafuta yaliyoganda mwilini. 

Chai nyeusi ambayo mara nyingi inatengenezwa na majani yaliyokauka na hpitia kiwandani na huwa na kiwango kikubwa cha coffeine. Chai hii ni nzuri kwani inasaidia msukumo wa damu huyo hivyo kukulinda kutopata magonjwa ya moyo na mshtuko. Pia wataalam wanasema chai ya aina hii inasaidia mapafu kwa wale wanaovuta sigara.
Wataalam wanasema pia aina nyingine za chai kama chai nyeupe inasidia kupunguza uzito na pia zinasidia kulinda meno yasioze.

ZIFUATAZO NI FAIDA ZA KAHAWA.
Mara nyingi watu wamekuwa wakiogopakunywa kahawa kwa madai kuwa kahawa inaleta magonjwa ya moyo na saratani ya tumbo. Lakini ukweli ni kwamba maneno hayo hayana mantiki kama utakunywa kwa kiwango staili.
Kahawa inasidia kuongeza kumbukumbu na kupambana na magonjwa yanayoshambulia moyo. Pia kahawa inapunguza uwezekana wa kupata saratani ya matiti na utumbo mkubwa. Wataalam wanaeleza kuwa kahawa inasaidia kuongeza kuupa mwili nguvu.
Ila kunywa kahawa kwa wingi sio vizuri kwa afya yako anasema DR Jane Scearce. Inaweza kusababisha kutopata usingizi na macho kuwa mekundu.
Waatalam wanashauri wanashauri unywe mc 400 kwa mwanaume na 300mc kwa mwanamke, ambayo ni sawa na vikombe 4 kwa mwanaume na 3 kwa mwanamke. Lakini kwa upande wa chai ni vikombe 6 kwa mwanaume na 4 kwa mwamke.
Coffeine inatoa faida nyingi za kiafya ikiwa na pamoja na kupunguza maumivu, uchovu na kukufanya kazi kwa mda mrefu. Pia inasaidia misuli kutoshikamana wakati wa mazoezi ya mwili.
Mwisho ingawa ingawa kuna faida nyingi za kunywa chai na kahawa sio vizuri kunywa kupita kiasi. Kunywa kwa kiwango kidogo kinachopendekezwa na wataalam kwa siku.
USIKOSE DARASA HURU LA KESHO.


Jumapili, 2 Novemba 2014

UHUSIANO



HATUA ZA KUFUATA KURUDIANA NA MPENZI WAKO WA ZAMANI-2.

 
Ndugu wasomaji wa makala zangu za uhusiano leo tunaendelea na hatua za kufuata ili kuweza kurudiana na mpenzi wako wa zamani. Hataua ya kwanza nilizungumzia makosa ya kuepuka ukitaka kurudiana na mpenzi wako ikiwa ni pamoja na;
(       (a)   kumpigia simu au kutuma sms kila mara
(       (b)   Kamwe usimwombe msamaha.
(c)  Usikubali kila kitu anachotaka
(d)   Usiendelee kuonesha kuwa unamjali
(e)   Usichukie ukigundua yupo na mtu mwingine.

Kama ulikua hujasoma hatua ya kwanza, basi isome kwenye blog hii kupata mtiririko mzuri.

Leo tuendelee na na hatua ya pili na ya tatu.
HATUA YA 2: USIWASILIANE NAE, JIPE MDA NA NAFASI.
Kuna kitu kinachoitwa ‘no contact rule’ kwa lugha ya wenzetu. Kanuni hii ni rahisi sana na inafanya kazi na yenye mafanikio makubwa. Kitu unachotakiwa kufanya ni kuacha kuwasiliana na mpenzi wako wa zamani kwa mda. Hapa na maana kwamba usimpigie. Kumtumia sms, kuchati nae twiter, facebook,whatsaap na mitandao mingine ya kijamii. Ukiweza futa namba zake kabisa na pia epuka kwenda sehemu ambazo mtaonana.
KWA NINI NISIWASILIANAE NAE?
(    (a) Mpenzi wako wa zamani anahitaji mda na nafasi kusahau maumivu yote baada ya kuachana, na hii itamfanya aanze kukumbuka. Watu wengi wanafikiri kwamba eti kama usipo wasiliana nae atakusahau kabisa, la hasha usipo wasiliana nae unampa mda wa kukumbuka wewe na atakuwa anajiuliza kwa nini haumtafuti?. 
  Hapa unatakiwa ukumbuke yale makosa niliyokuzuia kuyafanya katika hatua ya kwanza. Kitendo chako cha kutomtafuta kinakufanya usionekane mdhaifu bali ngangari na usiye na uhitaji mkubwa.

    (b) Wewe pia unahitaji mda na nafasi, kujitafakari na kujua wapi ulikosea. Unaitaji mda kutafakari kama kuna ulazima wa kurudiana na mtu aliyekuacha au la?Unaitaji kujifunza kama unaweza kuishi bila yeye. Unaitaji mda kujirizisha kuwa unaweza  kuishi ukiwa na furaha bila yeye.Ni kukumbushe kuna msemo usemao “Furaha haiji kwa kupata kitu ambacho huna bali kwa kukipenda kitu ulichonacho. 
(c) Lazima uwe mtu mwenye furaha kwa kipindi hiki cha mpito.
Unaitaji kuyathamini maisha yako kwa sasa. Hii itakusaidia pindi utakapokutana na  mpenzi wako baada ya “no contact period” avutiwe na wewe na kuona kuwa wewe ni mtu mpya.
 NISIWASILIANE NAE KWA MDA GANI? 
Kwa kawaida usiwasiliane nae mpaka pale utakapojiona kuwa umebadilisha maisha yako na unaweza kuendelea hata bila yeye. Kitaalam siku 30 zizatosha lakini unaweza kuchukua hata miezi 2 au 6 kutegemea na sababu zilizowafanya muachane.  
 Kitu cha muhimu hapa kwa kipindi hiki usije ukamwambia kuwa naacha kuwasiliana na wewe kwa mda fulani. Kitendo cha kutowasiliana nae sio ukatili bali ni kwa ajili ya afya ya akili na mwili wako. Kipindi hiki pia usipokee simu zake wala kujibu sms zake.

HATUA YA 3: JIJALI MWENYEWE
Sehemu hii ni muhimu zaidi ndugu yangu ni muhimu sana ndugu yangu. No contact(kutokuwasiliana) hakutakuwa na maana mpaka hapo utakapoamua kubadilsha maisha yako na kuwa bora zaidi. Jijali kwa;
(      (a) Badilisha muonekano wako na kuwa mzuri zaidi. 
   Badilisha muonekano wako, kimavazi kutakufanya uonekane wa thamani zaidi. Unaweza kubadilisha jinsi ya uvaaji, jinsi ya unyoaji ukawa wa kisasa zaidi na unayeendana na wakati. Unaweza kutengeneza mwili wako kwa kufanya mazoezi na kwenda gym. Hapa kuwa makini kidogo usije ukafanya vitu visivyokubalika miongoni mwa jamii inayokuzunguka au ukafanya kitu ambacho uwezi kukisahau kama kuchora tatuu.
(        (b)   Badilisha fikra zako na mawazo yako.
Kuwa mtu mwenye furaha na mwenye kujiamini ni jambo ambalo litakusaidia kurudiana na mpenzi wako. Mpenzi msomaji lazima utambue kuwa furaha ni kitu cha pekee ambachi kinatoka moyoni mwako na akilini pia. Vitu vinavyoweza kukupa furaha ni pamoja na kutoka out na marfiki zako, tembelea kumbi za starehe kama kuangalia sinema, kusoma vitabu vya ujasiria mali na kadhalika.
KWA LEO TUISHIE HAPA USIKOSE HATUA YA NNE.