Jumanne, 7 Oktoba 2014

DARASA LA MAPENZI


JINSI YA KUMFANYA MWANAMKE AKUPENDE

Wapo wanaume wanaozani kuwa kuna njia  za kutongoza la hasha hakuna formula maalumu za kutongoza kwa kuwa wanawake wanatofautiana kuanzia tabia, umbo na mwenekano. Ila kuna njia za kumfanya mwanamke akupende, akutake, akutamani na ikibidi akutongoze kabisa. Hivi unajisikiaje mtoto wa kike akikuambia anakupenda au kwa lugha rahisi akikutongoza.? Bila shaka utajisikia kidume tena kidume cha mbegu. Nsikuchoshe ngoja nikupe njia.

(          1.  JIJALI NA KUJIPENDA MWENYEWE
Bila shaka muonekano wa nje ni muhimu zaidi kuliko kitu kingine chochote. Ebu nikuulize swali hivi kuna mwanaume anayeweza kuvutiwa na kumtongoza msichana mchafu anayenuka na kuvaa ovyo ovyo? Kama jibu ni hapana ndivyo ilivyo kwa wasichana pia hakuna mwanamke anayependa au kuvutiwa na mvulana anaevaaa ovyoovyo, hasiyependa kujitunza na kujithamini. Kuvaa vibaya, kuwa mchafu ni ishara ya ushamba na siku zote ushamba unawaboa kinadada. Upo hapo sio unanitolea mimacho tu mwanaume mzima unavaa mlegezo. Cha msingi ni kujijali mwenyewe kuanzia chakula, malazi na mavazi. Sasa kama unakula hovyo hovyo lazima utaonekana ovyo ovyo (garbage in, garbage out). 

Fanya mazoezi kuweka mwili wako vizuri . kumbuka mwanamme aliyejengeka misuli vizuri ni kivutio kwa wadada na kwa kuwa wanaongozwa na hisia basi hata kwenye tendo la ndoa huisi kufikishwa kileleni na wanaume wenye afya njema. (sasa sio ukapige jimu ambazo hazijapimwa ukajazia upande mmoja wa kifua na kwingine ukabaki njiti mimi simo) Lakini nazani unanielewa fanya mazoezi  mara kwa mara.

          2. KUWA MTU WA WATU
Usipende kukaa mwenyewe jitahidi kujichanganya na watu wa aina mbalimbali hasa wasichana warembo na kwa kufanya hivyo utapata na kujifunza njia za kuishi na wasichana utajua nini wanapenda na nini hawapendi kufanyiwa.Waone wasichana kama rafiki zako lakini kuwa makini usiwe mwongeaji sana maaana utakuwa used and boared. Msichana yeyote anavutiwa na kupenda mvulana au mwanaume anayeshirikiana na watu wa aina mbalimbali na hii ni ishara kuwa hatokuwa mpweke pindi mtakapo kuwa kwenye mahusiano .

(             
             3.  KUJIAMINI NI SILAA
Linapokuja suala la kujiamini hata mwanaume awe mbaya kiasi gani kama anajiamini lazima atakuwa kivutio kwa wasichana wanaokutana nae. Wasichana siku zote wanapenda ulinzi, mtu ambae atakuwa kinga yake sasa ushawai kuona mlinzi hajiamini? Kujiamini ni ngao kwa sabababu wanaume wanafanana kwa vitu vingi kwa mfano mavazi yao huwa hayawatofautishi sana, kwa hiyo kwenye kundi la wanaume wanaovaa sawa lazima mwanaume anayejiamini ataonekana wa kipekee zaidi. Kujiamini kunamfanya mwanamke ajihisi kuwa salama pindi atakapo kuwa na wewe kwa hiyo wanavutiwa sana na wanaume wanaojiamini tupilia mbali sura na uhandsomboy. Badilika ndugu jiamini na kujikubali jinsi ulivyo.

             4.   ONESHA HISIA ZAKO KWA UMPENDAYE
Kwa mila na tamaduni zetu za kiafrika hata mwanamke awe anakupenda vipi ni ngumu kusema kuwa anakupenda. Cha msingi kama umegundua kuwa anakupenda na wewe unampenda ni vizuri ukafunguka kuliko kukaa kimya kwani kukaa kimya kutamfanya aone huna hisia na yeye hivyo kuwa mbali na wewe. Ila kuwa makini sio kwa sababu anavutiwa na wewe basi ukamtongoza tuu ata kama sio chaguo lako hiyo ni dhambi kubwa. Wakati mwingine msichana anaweza kuvutiwa na wewe kwa jinsi ulivyo na confidence, very attractive and sexuality lakini akakuchukulia kama rafiki wa kawaida tu kwa hiyo kwa kuonesha hisia zako kwake utakuwa umevunja mipaka ya urafiki na kuingia kwenye mahusiano...
 
 

Leo tuishie hapa next time tutaangalia                   
DALILI ZA MWANAMKE ANAYEKUPENDA. Don’t misss.....

0 comments:

Chapisha Maoni