ZIJUE AINA NA MAKUNDI YA
WATU DUNIANI
Tafiti
mbalimbali zinaonesha kuwa kuna watu wa aina tofauti hapa duniani. Ni vizuri
kujijua upo katika kundi gani na kama ni kundi baya basi kuna hatua za kuchukua
kujiondoa katika kundi hilo.
1.
WATU AINA YA SANGUIN
Hili
ndilo kundi kubwa la watu, ni kwamba hawa ni watu ambao hawana maneno mengi.
Hata uwezo wao pia wa kupambanua mambo ni wa kawaida, wanapenda kwamba
wanapoongea jambo uwe una msikiliza. Pia watu hawa ni maarufu wa kueleza
mipango yao ya kimaisha ingawa baadhi yake huwa haifanikiwi. Wale watu
wanaopenda kuigiza na kuchekesha wapo kwenye kundi hili. Pia watu aina ya
Sanguini ni watu wenye roho nzuri sana. Kama ni mwanamke yupo kwenye kundi hili
basi ni ngumu sana kumshawishi kwa maneno na kufanikiwa kumpata.
2.
WATU AINA YA MELANCOLIN
Hawa
ni watu wenye uwezo mkubwa wa kupambanua mambo na kama wapo darasani huwa wana
uwezo mkubwa wa masomo magumu kama sayansi na hesabu. Watu wa kundi hili huwa
na huruma sana lakini wanasumbuliwa na tatizo la kutojiamini ingawa
wanachokisema mara nyingi huwa na mashiko. Baadhi yao huwa wanakata tamaa
haraka na huwa hawapendi kuvunja sheria. Pia ni wagumu wa kusahau lakini wepesi
wa kuadhibu na kuhukumu. Ni wasiri mno japo uongozwa na uaminifu na ukweli.
3.
WATU AINA YA FLAGMENTIC
Watu
wa kundi hili mara nyingi hawana msimamo na ni wepesi wa kuharisha mambo, kwa
mfano kama ni mwanamke anaweza kuamua kupika wali lakini akimaliza tu kupiga
mboga anabandika sufuria la ugali. Ni wadadisi sana na wana uwezo mkubwa wa
kukaa na siri moyoni. Wanaweza kujenga hoja na wakati mwingine kubadili ukweli
kuwa uwongo au uwongo kuwa ukweli. Watu wa kundi hili wanaumizwa sana na
mapenzi na wengi wao hawapo kwenye ndoa ni wepesi na kuacha na kutoa talaka.
4.
WATU AINA YA COLERICK
Watu wa kundi hili wanapenda sana kutawala
wenzao ingawa uwezo wao wa kiakili ni wa
kawaida. Watu wa kundi hili wanajiamini kupita kiasi, hawapendi kuongea
ongea wala kucheka cheka hovyo. Hili ni kundi la watui matajiri sana duniani
ambao hata wakikusaidia ni kwa malengo ya kupata faida zaidi. Watu wa namna hii
mara nyingi hawapendi sana starehee.
KAZI
KWAKO KUJUA UPO KUNDI GANI.........Usikose DARASA HURU
la kesho.
0 comments:
Chapisha Maoni