Jumatano, 22 Oktoba 2014

DARASA LA MAPENZI



ZIFAHAMU FAIDA ZA KUFANYA MAPENZI

Kila kitu dunian kina faida na hasara ingawa wengi wanazani kuwa tendo la ndoa ni kwa ajaili ya kujifurahuisha tua au kuzaliana. Ni weke wazi lengo langu si kuhamasisha watu wafanye ngono kwani ukimwi upo na unauwa. Wataalam wa mambo ya afya wamefanya utafiti na kugundua kuwa zipo faida za tendo la ndoa au kufanya mapenzi kwa maneno mengine kama tu yatafanywa kwa utaratibu maalum. Zifuatazo ni baadhi ya faida.

Kiafya.
Wataalam au wanabailojia wanadai kuwa kufanya mapenzi ni moja kati ya mazoezi ya mwili. Endapo mtu atafanya tendo hilo mara tatu kwa wiki kwa mda wa mwaka mzima ni sawa na kukimbia mail 75. Kama watu wakifanya mapenzi kwa mda wa nusu saa tendo hilo uongeza vizalisha nguvu 150 na hii ni sawa na kukimbia dakika 15 kiwanjani. Kwa hiyo tendo la ndoa ni mazoezi tosha kwa mwanadamu kama atalifanya kwa utaratibu.

Kuongeza msukumo wa damu.
Kufanya mapenzi husaidia kuongeza kasi ya mtiririko wa damu kwenye ubongo na sehaemu nyingine ya viungo vya mwili na hii huchangia kuongeza kasi ya mapigo ya moyo na kupumua ambavyo huboresha mzunguko wa damu mwilini.

Kadri kiasi cha damu mpya mpya yenye oxegen na homoni inapofikia chembechembe za damu, viungo na misuli inatumika katika zoezi la uunguzaji wa chakula na damu iliyotumika inapoondolewa, pia kiasi cha uchafu hutolewa ambacho ungesababisha misuli kushindwa kufanya kazi na hivyo kusababisha maumivu ya mwili.

Hupunguza mafuta yenye kileo (Cholesterol).
Kufanya mapenzi kwa mpangilio kutakusaidia kuweka sawa uwiano wa mafuta yenye kileo(Cholesterol) nzuri na cholesterol mbaya na wakati huo huo hupunguza kwa ujumla kiasi cha mafuta yenye kileo mwilini.
Kupunguza maumivu.
Wakati wa kufanya mapenzi homoni iitayo Oxytosin huzalishwa mwilini ambayo husababisha kuzalishwa kwa homoni iitwayo Endrorphin ambazo husaidia kupunguza maumivu kama vile kuvimba sehemu za viungo(Arthritis) maumivu ya shingo (Whiplash) na maumivu ya kichwa, kiuno na mgongo. Hivyo basi unaweza kujitibu mwenyewe magonjwa yaliyotajwa hapo juu sio kukimbilia kunywa dawa.

Hupunguza baridi na mafua.
Wataalam wanasema kuwa wanaofanya tendo la ndoa mara moja au mbili kwa wiki huonesha 30% ngazi ya juu ya ulinzi wa mwili uitwao Immunogloulin, ambayo inaongeza kinga mwilini.

Kuonekana kijana na kuishi mda mrefu.
Wataalamu wanabainisha kuwa wakati wa tendo la ndoa kuna homoni iitwayo Dhea huzalishwa. Hii husaidia msisimko wa mapenzi kuongezeka. Dhea ni kemikali ambayo husaidia kuweka sawa kinga ya mwili, huongeza hufahamu, kuimarisha mifupa, kuimarisha afya na mishipa ya moyo (Cardiovascular) na pia hufanya kazi ya kulinda mishipa ya fahamu.

Huongeza uzalishaji wa Homoni za kike (Oestogen) na za kiume (Testosterone).
Kufanya mapenzi kwa mpangilo maalumu huongeza uzalishani wa homoni tajwa hapo juu ambazo huimarisha mifupa na misuli. Madaktari wanabainisha kuwa homoni za kiume huufanya moyo uwe na afya na kuwa na mafuta yenye kileo (Cholesterol) mazuri kuwa mengi, kwa wanaofuatila zaidi nshataja kazi yake hapo juu. Tendo la ndoa humwongezea mwanamke homoni ya kike(Oestrogen).
kutunza tissue za sehemu ya uke na pia kuulinda mwili zidi ya magonjwa ya moyo. Homoni hii umwongezea mwanamke hisia hivyo kuwajibika vizuri wakati wa tendo la ndoa.


 

KWA LEO TUISHIE HAPA, USIKOSE DARASA LA MAPENZI LA KESHO.

0 comments:

Chapisha Maoni