JINSI YA KUFANYA NYWELE
ZIKUE KWA HARAKA.
Moja
ya imani kubwa iliyojengeka miongoni mwa waafrika hasa watanzania ni kwamaba
nywele nyeusi hazikui kwa urahisi kama aina nyingine za nywele kama za wazungu,
wahindi na waarabu. Ukweli ni kwamba nywele aina zote zinakuwa kwa wastani wa
nusu inchi kwa mwezi anasema DR Del Sandeen mtaalam wa nywele nyeusi. Wanawake
wengi wenye nywele nyeusi wamakuwa wakiteseka sana mpaka kufikia hatua ya
kuzikata nywele zao au kuvaa nywele za bandia (wigi). Hakuna haja ya kuteseka
kwani kinachoitajika ni kufuata njia na mbinu zitakazo kutoa kwenye tataizo
hili. Zifuatazo ni njia utakazotumia ili kuzifanya nywele zako ziwe zenye afya
ndefu na kuvutia.
1.FUATA KANUNI ZA AFYA/KULA VIZURI
Kabla
ya kutibu tatizo kwa nje inatakiwa kulitibu kwa ndani. Ni ukweli kwamba vitu
unavyokula, kunywa na jinsi gani unautunza mwili wako vina mchango mkubwa
katika ukuaji wa nywele zako. Nywele zina Keratini ambayo ni protini
inayotengenezwa na amino acid. Ili nywele mpya ziweze kukua, mwili wako unaitaji
uzalishe acid inayoitwa amino acid. Kwa hiyo vyakula vyenye proteini ni muhimu
kwa ukuaji wa nywele zako. Akikisha unakula vyakula vyenye protini kwa wingi
kama mayai, nyama, maharage, samaki na kadhalika.
Unatakiwa
ule matunda, mboga za majani, kunywa maji mengi na kufanya mazoezi mara kwa
mara. Kwa kuwa nywele zako zinakuwa kutoka katika mwili, unapoutunza mwili wako
vizuri, jua kua nywele zako, ngozi na hata kucha zinanufaika pia.
Kula
vyakula vyenye vitamin C na mbogamboga kama spinachi. Mwili wako unatumia
Vitamin C kutengezeza kitu kinachoitwa kitaalam Collagen, ambacho ni muhimu
sana kwa ukuaji wa nywele. Vitamini C pia inasidia kupunguza madini ya chuma
amabayo ni kikwazo kwa ukuaji wa nywele.
Utafiti
unaonesha kuwa watu wanaokumbwa na tataizo la upungufu wa Vitamini na kutokula
au kufuata lishe bora mara nyingi wanapatwa na tatizo la kuwa na nywele kavu na
zisizorefuka.
2.TUMIA MAFUTA YA KULAINISHA
Kiasili
nywele nyeusi ni kavu sana hivyo basi unashauriwa kutumia mafuta kuzifanya ziwe
laini. Hapa namaanisha utumie shampoo au air conditioner zilizotengenezwa kwa
ajili ya nywele kavu. Zingatia kuwa sio kila mafuta ni mazuri kwa nywele zako
kwa sababu kila aina ya mafuta yanatengenezwa kwa ajili ya aina fulani za
nywele. Kwa mfano kuna mafuta kwa ajili ya nywele kavu na pia kuna mafuta kwa
ajili ya nywele zenye mafuta. Hapa wanawake wengi wanakumbwa na tatizo hili na
kujituta wanapaka mafuta wasiyojua yametengenezwa kwa ajili gani. Usipake
mafuta kwa kuwa shostito wako amepaka, bali chunguza nywele zako zipo kwenye
kundi gani.
3.PUNGUZA NYWELE ZAKO MARA KWA MARA
Kwa
kawaida nywele zinakuwa kutoka kwenye mizizi, nywele zilizoharibika zinazuia
ukuaji wa nywele mpya hivyo unashauriwa kuzikata nywele zilizoharika kuruhusu
nywele mpya kukua. Unashauriwa kukata nywele zako kila baada ya wiki 6 mpaka 10
kwa wastani wa robo inchi au nusu inchi na sio zaidi. Kama anayekuset na
kukutengeneza anasisitiza kukata nywele zako kila unapokwenda saloon jua kuwa
nywele zako zinaweza zisiwe kubwa. Cha msingi ni kutafuta mtaalam anayejua ni
kiasi gani cha nyele kinatakiwa kupunguzwa na ni kwa mda gani na pia ni vizuri
kujifunza jinsi ya kupunguza nywele zako. Kumbuka kuwa ukataji holela wa nywele
kunasababisha matatizo ya nywele kukua na kuwa mbaya.
4.TUNZA NYWELE ZAKO KWA UMAKINI
Hii
ni pamoja na kupunguza matumizi ya kemikali, kutumia vitu vyenye joto kali(heat
treatment) na pia kuosha mara kwa mara. Jaribu kupunguza mitindo yenye joto
kali, chagua staili ya nywele ambayao haitengenezi sana joto. Unashauriwa uoshe
nywele zako mara tatu kwa wiki na kwa kutumia maji ya moto. Hair messaging inasaidia
ukuajia wa nywele kwa sababu inasaidia kuongeza msukumo wa damu na kupeleka
virutubisho muhimu kwenye nywele zako.
Usitumie rubberband
kufunga nywele zako.
Kama
unataka kufunga nywele zako na kuzibana kwa nyuma usitumie rababendi au kamaba,
badala tumia kibanio. Kibanio kinasidia kuzuia nywele zisijizibe sehemu ya
kutokea hivyo kukua kwa urahisi
Usizichanae sana
nywele zako.
Hakuna
haja ya kuzichana nywele mara 100 kila siku kwa sababu ukweli ni kwamba
usipozichana mara nyingi ndivyo zitakavyokuwa kwa urahisi. Chana nywele zako
zinapokuwa kavu na sio zikiwa na majimaji au unyevunyevu.
5.TUMIA STAILI ZA KUZILINDA NYWELE ZAKO
Ni
tataizo kwa watu wengi kuwa pindi nywele zinapokuwa kubwa wanapenda kuziachia
ili watu wazione ni kubwa kiasi gani. Pia wanawake wengi wanapenda pia kuziacha
zipigwe na upepo. Lakini tambua kuwa kutumia mitindo ya kuzilinda kutakusaiodia
kuzibakisha kwenye ukubwa wake. Mitindo ya kuzilinda kutakusaidia kuzuia nywele
zako zisigusane na nguo, mito au siti ya gari. Kwa kuzifunika nywele zako
kutakusaidia kutunza unyevunyevu wa nyele zako na kuzuia ukavu unaosababisha
madhara. Funika nywele zako hasa wakati wa kulala.
KWA
LEO TUISHIE HAPA, USIKOSE KONA YA UREMBO NA TUTAZUNGUMZIA NJIA ZA ASILI ZA KUTUNZA NYWELE ZAKO........Tchaooooooooooooooo.
0 comments:
Chapisha Maoni