Alhamisi, 23 Oktoba 2014

LOVE STORY




EVERLASTING LOVE (Penzi la milele)
SEHEMU YA 4
MTUNZI: ELIAS ADOLF(eliado)
ILIPOISHIA
Wazazi wake Rachael wamerudi kutoka Arusha walipokuwa wakienda mapumzikoni na hii ni baada ya kupata taarifa za msiba wakiwa njiani, mama yake Rachael anaingia chumbani kwa mwanaye na kukuta Rachael yupo juu ya mwanaume wakivunja ile amri ngumu ya sita..Tiririka....

Basi watafanya nini hili hali mtoto akiunyea mkono huwezi kuukata, wanamgombeza sana na Emmanuel anatishiwa kuuwawa na bastola na baba yake Rachael lakini kwa huruma ya mama Rachael anafanikiwa kumtoa nje na kumwambia apotee eneo hilo haraka.
Majuto ni mjukuu, roho inamuuuma sana Emmanuel lakini hana jinsi maji yakishamwagika hayazoleki, kichwa chini, mikono kichwani utamu umegeuka shubiri, anafika kwao anapokelewa na maneno makali sana kutoka kwa mama yake mkubwa siunajua tena mtoto huyu yupo masomoni jijini hapa nyumbani kwao ni kule Dodoma.
Huku nyuma baba na mama yake Rachael wanapanga kumwamisha shule mtoto wao kutokana na matukio yanayoendelea kutokea, kimoyomoyo walikuwa wakiyakumbuka maneno wa marehemu Mbunda wa Mbunda aliyetabiri juu ya maisha ya huyu mtoto lakini imani ya dini iliwafamya kujisahulisha.
 Rachael alichanganyikiwa kwa penzi la mtoto wa askofu na hata wazazi wake walijiuliza sana bila kupata jibu. 
Walishauriwa na mwalimu wa malezi kuwa wasubiri mwaka huo uishe kwani zilbaki wiki tano tu kabla ya kumalizika kwa muhula wa pili ili atakapohamia akaanze kidato kingine, bila kinyongo walikubaliana na ushauri huo na walimsihii Rachael ajitaidi kufanya vizuri. 
kwa hiyo ndani ya mwezi huo mmoja watoto hawa wadogo lakini wenye mambo makubwa waliendelea na mahusiano yao ya kimapenzi kama kawaida. Sasa hivi walibadili staili ya kulimenya tunda walikuwa wanasubiri wikiendi na wanakwenda kwenye nyumba za wageni na kufanya utundu wao.
Baada ya mwezi ule wa mitihani kumalizika Rachael alikuwa anasubirri ifike january ya mwaka mwingine apate kuama shule kwani hata yeye ingawa alikuwa akimpenda sana Emmanuel lakini alikuwa amechoshwa na malalamiko ya wazazi, waalimu na wanafunzi wengine kuwa yeye hajatulia, akijaribu kulinganisha na uvumi uliozagaa wiki moja kabla ya mitihani eti yeye aligawa penzi kwa mwalimu wa hesabu ili apewe majibu. 
Roho inamuuma sana kwani zile zilikuwa njama zilizopangwa na Juliet msichana aliyetokea kumpenda sana boyfriend wake. Kwa kiasi kikubwa skendo hii ilifanikiwa kwani Emmanuel hakuwa tayari tena kuendelea na Rachael na likizo hii aliamua kurudi kwao Dodoma kuwasalimia wazazai wake.

RACHAEL AHAMIA SHULE MPYA
Tarehe 13/01 Rachael anaripoti katika shule ya wasichana iliyopo morogoro wilayani mahenge ulanga, shule hiyo iitwayo ST AGNESS GILRS SECONDARY SCHOOL iliyo chini ya parokia ya kwiro jimbo la mahenge pia chini ya muhasham baba askofu Agapty Ndorobo. 
Shule hii ni nzuri kiupande wa maadili kwani watoto wa pale wanalelelwa katika misingi ya kidini. Rachael anapokelewa na na matroni Maria ambaye ndio sister mlezi wa shule hiyo pia anakabiziwa kwa mwanafunzi mwenzake kama mwenyeji wake aitwaye LUCY MASIMBI huyu wanatokea kuzoeana sana kutokana na uchangamfu wake.
Maisha yanaendelea vizuri kwa Rachael japokuwa inaonekana kama ngumu kwake kwani kuamka ni saa kumi na moja na ifikapo saa kumi na mbili wanafunzi wote wanatakiwa wawe kanisani haijalishi ni muislamu au mkristu, maadam upo pale unatakiwa kufuata shughuli na ratiba za pale.
 Na kila saa sita mchana na saa kumi na mbili jioni watu wote husimama na kusali ile sala ya malaika wa bwana kwa wale waamini wa kikatoliki wanajua sala hiyo. Masomo yanaanza kama kawaida saa mbili asubuhi na ifikapo jioni kuanzia saa kumi na moja jioni huwa wanakwenda bustanini iliyo kidogo chini ya shule hiyo basi huko ndipo Rachael huwa anafurahi.
 kwani hupata nafasi ya kuonana na wanaume au wavulana ingawaje huwa hapati nafasi ya kuongea nao lakini kwake huwa ni zaidi ya faraja. 
Sehemu hiyo kuna uwanja wa mpira wa miguu hapo huwa wanafanya mazoezi wavulana wa aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na wale wa shule ya wavulana iitwayo Kwiro boys high school, hii ni shule kongwe iliyoanzishwa na wajerumani na watu wengi maarufu walishawahi kusoma hapo.
Zamani ilijengwa kwa makusudi ya kidini lakin mwaka 1967 iliitaifishwa na serikali, ina wanafunzi wengi sana na wanatoka karibu mikoa yote ya nchii hii , inasifika kuwa na mahabara nzuri sana licha ya hayo mazuri pia ina sifa kubwa ya kuwa na fujo na vurugu. 
Miaka ya nyuma iliripotiwa wanafunzi wa hapo walishawahi kuchoma mabweni na kupiga mawe msafara wa mkuu wa wilaya. Kwa hiyo hata hiyo shule ya kina Rachael walikuwa wakiwaogopa sana.
Kuna baadhi ya wanafunzi wa shule hizi mbili walikuwa na mahusiano mazuri ya kiuwanafunzi lakini wengine wao ni mapenzi tuu na kusahau kilichowapeleka huko. 
Kuna mwanafunzi mmoja jina lake Resty huyu alikuwa na kaka yake hapo Kwiro secondary waliishi kwa raha sana na kila siku walikuwa wakionana kisiri na kusalimiana, kaka yake huyo alipata umaarufu sana kutokana na the way jinsi alivyo alikuwa tozi sana na muongeaji sana kwa hiyo alijuana na mabinti wengi sana wenyewe walimwita SNOGA, huyu jamaa alikuwa na kipaji cha kucheza ile miziki ya kizungu kama vile hana mifupa hapa huwa namkumbuka marehemu Michael Jackson. 

Kwa kuwa Rachael alikuwa anatamani sana kupata rafiki wa kiume kutoka kwenye shule hiyo, alianza kazi hiyo mara moja bila mafanikio baadae alipotafakari sana aliona kuwa kulikuwa na aja ya kuunda urafiki na Resty dada wa yule tozi (Snoga bowow). Kwa kuwa siku zote penye nia pana njia, Rachael alifanikiwa kuwa na urafiki na Resty, lakini kwa mda mfupi tu Resty alifanikiwa kuisoma vizuri tabia ya rafiki yake na kugundua kuwa sio nzuri.
 
Kwani ni juzi tu Rachael alishafanikiwa kumwingiza mfanyakazi wa shule yaani mtunza bustani katika himaya yake ya utumwa wa mapenzi na kumsababishia mvulana huyo kufukuzwa kazi kwa madai ya kuwa na ukaribu na baadhi ya wanafunzi wa hapo.
Kwani alishawahi kufumwa na Rachael huko bustanini wakifanya vitu vya ajabu, sitaki kulielezea sana tukio hili kwani vitu vya Rachael si mnavijua ana maufundi ya ajabu. 
Alifanikiwa kuwa karibu sana na Snoga lakini alishindwa kumuingiza kwenye himaya yake kwa sababu mtanashati huyu alishaonywa na dada yake juu ya tabia mbaya ya Rachael. Ingawa kwa upande wake aliona kama anazibiwa bahati tuu, na alijisemea kimoyomoyo kuwa akiingia anga zangu kwa uzuri aliokuwa.................

0 comments:

Chapisha Maoni