Jumatano, 8 Oktoba 2014

LOVE STORY



EVERLASTING LOVE  (Penzi la milele) -1

MTUNZI : ELIAS ADOLF (eliado)
UTANGULIZI.
 
Ni siku ya furaha kwa familia ya mzee Kijoji, siku ambayo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa, siku ya vifijo,vigelegele na shangwe. Siku ambayo haitasaulika kwa mwanaye mpendwa kupata jiko baada ya kutoka masomoni nchini India. 
Ghafla siku hiyo ya furaha inaingia doa baada ya kusikika kwa mlio mkali wa risasi iliyopigwa hewani ikiambatana na sauti ya kukoroma ya msichana mrembo aitwae RACHAEL. Msichana huyo huku akiwa amedondoka chini mita chache kutoka lango kuu la kuingia kanisa la Mt.Joseph, mahali ambapo ndoa ya mpenzi wake wa zamani ALEX na EASTHER ilikuwa ikifungwa. 

Maneno machache yalisikia “please Alex dont leave me alone, penzi langu kwako ni penzi la milele elewa bado nakupenda yote yaliyotokea yalipangwa, ebu kumbuka tulipotoka”,ghafla msichana huyo mrembo anazimia. ALEX anatoka nduki huku akitupa pete ambayo alitakiwa kumvalisha EASTHER na kwenda kumkumbatia RACHAEL. 
Ndipo hapo harusi inaingia doa nakuwaacha watu wote midomo wazi, kwa bahati nzuri JACKSON mwandishi wa habari wa kimataifa aliyeripotiwa kupotea akiwa Dubai siku chache kabla ya harusi yake na EASTHER alipokweenda kufanya shopping yake ya harusi anatokea na kwenda kumkumbatia bibi harusi EASTHER.
 Watu waliokuwa wakimjua mwandishi huyo wa habari walishikwa na butwaa kwani inaaminika kuwa alitekwa nyara na alishauwawa. 

Patashika nguo kuchanika askari polisi nao wameshafika eneo la tukio kutokana na mlio wa risasi uliosikika, ama kweli kupenda kubaya na akupendaye hakuachi. JE, NINI KITATOKEA, Jackson alikuwa wapi miaka yote hiyo na kwa nini ALEX alikwenda kumkumbatia Rachael na kumwacha bibi harusi Esther. Ungana na mwandishi wako ELIADO katika simulizi hii kali na ya kusisimua.*********************************
 
RACHEAL ANAZALIWA.
 
Ilikuwa siku tulivu na yenye furaha kubwa kwa familia ya mzee MBUNDA, familia tajiri na yenye watu wenye taaluma mbalimbali kama vile udaktari, uandisi, upadri na wengine walikuwa viongozi wa kisiasa katika serikali ya wakati huo. Furaha hiyo ilitokana na kuzaliwa kwa mtoto wa kike wa pekee aliyepewa jina la RACHAEL

Rachael ni mtoto wa tatu katika familia hiyo na ni yeye tu ndio wa kike kwa hiyo alitokea kupendwa sana. Kwa kumbukumbu ilikuwa tarehe 14/03/1990 mwaka unaosemekana ulikuwa wa mavuno mengi, ilifanyika tafrija kubwa sana iliyoudhuriwa na watu wa aina mbalimbali pamoja na babu yao mkubwa aliyeitwa Mbunda wa Mbunda mzee huyo ni mtabiri wa nyota na mambo mbalimbali ya kimaisha kama mavuno mvua na njaa. 

Alishawahi kutabiri kuwa Tanzania itavamiwa na Nduli Iddy Amin na ikatokea hivyo, isitoshe alishawahi kutabiri juu ya kifo cha askofu mmoja wa jimbo la Mahenge na siku chache baadae askofu huyo alifariki mtoni kilombero walipokuwa wakivuka kwenda Ifakara. Labda nikudokeze kitu kimoja mzee huyu alikuwa na uwezo wa kugeuza mchanga kuwa sukari au chumvi, maji kuwa pombe na mengineyo mengi ya maajabu.  
                                 
Na kipindi Rachael anazaliwa mzee huyo alikuwa hana hata jino moja kwa maneno mengine tunawezasema alikuwa mzee sana yaani kibogoyo na hata kuongea kwake ilikuwa kwa tabu sana. kilichokuwa kinasubiriwa hapa ni mzee huyo aliye heshimika sana na kuogopwa kutoa utabiri wake juu ya kuzaliwa kwa mtoto huyu.  
                                     
Mzee Mbunda alisimama na kusema” wote mulilo hepa nawafilendiile mpaka kumoyo” yaani wote walio pale anawapenda sana kutoka moyoni akaendelea kusema ninafuraha kubwa sana kutoka moyoni. 
Lakini niseme jambo moja la msingi nalo ni kwamba mtoto huyu aliyezaliwa atakuja kuteseka sana katika maisha yake kwa sababu ameingiliwa na pepo la ngono, na kwa maana hiyo atakuja kuteseka sana pindi atakapo balehee na atakuwa anapenda sana kufanya mapenzi na hii inatokana na mama yake kutotii masharti ya mizimu. 

Si mnakumbuka alivyopata tu ujauzito wa huyu mtoto alitakiwa kwenda Mahenge Ulanga kuondoa mkosi akapuuza, kwa hiyo mizimu imeamua kufanya makusudi mpaka hapo itakapotimiziwa ahadi yao ya kufanyiwa tambiko kubwa sana. Mimi kama mzee wa ukoo wa Mbunda wa Mbunda ninashauri baada ya miezi sita mfike Mahenge kwa msaada zaidi. Alimaliza mzee huyo na kukaa kwenye kiti chake.
 
Watu wote waliingiwa na huzuni na hofu kubwa kutokana na maneno hayo, kimya kikuu kilitawala mpaka hapo Padre Fransisi aliposimama na kuamua kuvunja ukimya kwa kusema”Jamani ndugu zangu wapendwa katika kristo, tumsifu yesu kristu” 

baada ya watu wote kuitikia kwa unyonge aliendelea kwa kusema mambo hayo yaliyoelezwa na mzee wa ukoo yapo kwani hata vitabu vitakatifu vya mwenyezi mungu vimeelezea juu ya mapepo wabaya. 
Cha msingi ndugu zangu wapendwa katika bwana ni tumwombe mungu avunje roho zote za mizimu na roho za pepo wabaya wanaoweza kumwingia mtu na kumfanya mtumwa wa dhambi. Baba mungu wa mbinguni aishie na kutawala amlinde na kumwepusha mtoto huyu na hatari zote za roho na mwili. 

Baada ya kumaliza kusema hayo na yeye aliamua kukaa kwenye nafasi yake.Kutokana na kauli hiyo kuna watu walionekana kuliafiki hilo na wale wenye imani haba walipinga na kusema cha muhimu hapo ni kufuata yale yaliyosemwa na mzee wa ukoo, kwa hiyo kulitokea pande mbili zinazovutana wale wanaokubaliana na ushauri wa mzee wa ukoo na wale wanokubaliana na ushauri wa padre Fransisi. 

Ulitokea mvutano wa hapa na pale lakini baba wa mtoto alisimama na kusema suala hilo ni dogo sana yeye na mkewe watalimaliza na kujua nini cha kufanya, aliendelea kuongea na kusema leo ni siku ya furaha kwa hiyo haina haja ya kulumbana kwa jambo ambalo halijatukusanya hapa. 
Pia akaongeza kwa kusema isitoshe huo ni utabiri tu au hamjui maana ya utabiri, basi yaacheni hayo tuendelee na kilichotukusanya hapa. 
Basi tafrija ikaendelea kwa wale wanaokunywa pombe wakanywa za kutosha yaani ushindwe mwenyewe na wale wa nyama choma nao kama kawaida na pia wale wa vinywaji laini nao hawakutengwa.
 
Tafrija iliisha na watu wakatawanyika na kuendelea na shughuli zao za kila siku. Wale wa mbali kama mahenge walilala na kuondoka kesho yake. Huku nyuma familia ya mzee Mbunda ilikaa kikao na kujadili swala lililojitokeza na nini kifanyike. 


Kilichokuwa kikiwapa wakati mgumu ni historia ya mzee yule wa ukoo kutabiri vitu na kutokea. Lakini kwa kuwa na wao walikuwa ni watu wa imani ya dini waliamua kupuuzia kwa kusema mambo hayo yapo lakini kwa uwezo wa mungu muumba mbingu na vyote vilivyomo yote yatakwisha. Hivyo suala hilo lilifutika vichwani mwao na wakaendelea na shughuli zao kama kawaida.

Kabla ya miezi sita aliyoisema babu yao mzee wa Mbunda wa Mbunda kufika mzee huyo aliitikia sauti ya mungu iliyomtaka aende akapumzike pumziko la milele. Hivyo alifariki tarehe 15/06 mwaka huo huo. Kama kawaida ya watanzania na waafrika kwa ujumla shughuli za mazishi ziliendelea na baada ya wiki moja marehemu aliifaziwa kwenye zizi lake la milele au kwa maneno mengine nyumba ya mapumziko. 

Vilitokea vitu vingi vya ajabu katika mazishi ya mzee huyo lakini watu hawakushangaa sana kwani kwa watu maarufu kama hao, moja ya maajabu hayo ni pamoja na kutotosha kwa jeneza kwenye kaburi lililochimbwa pia ilinyesha mvua kubwa iliyoambatana na radi kali sana iliyopelekea watu saba kupoteza maisha yao na kwa maoni ya wenyeji walidai kuwa eti waliokufa walimsindikiza mfalme huyo. Hivyo baada ya siku arobaini................................................................................................................
ITAENDELEA

0 comments:

Chapisha Maoni