Alhamisi, 23 Oktoba 2014

UHUSIANO



JINSI YA KUFANYA MWANAMKE AJISIKIE SPECIAL
 
Hakuna mwanaume hasiyependa mchumba wake, mkewe au girlfriend wake ajisikie special. Hivi unajua ni kwa kivipi? Acha leo nikueleze ni nini hasa mwanamke anahitaji and how real men can make it. Zifuatazo ni njia mbadala
(1) JUA NINI ANAHITAJI
Ni ukweli wa asili (fact of nature) kwamba wasichana huwa wanahitaji kitu fulani kutoka kwa mwanaume. Najua ni ngumu kwa mwanaume kujua vitu hivyo kwa sababu vipo ndani ya ya mioyo ya wasichana. 
Huwezi kuepuka ukweli huu, cha msingi mwanaume anatakiwa kujifunza na kujua nini mwanamke anahitjai kutoka kwake, kwa hiyo ukijua kwa undani au kwa kiasi kikubwa nini msichana anahitaji ndivyo ilivyo rahisi kumfanya yeye ajisikie special. 
Ni ukweli usiopingika kwamba sio wasichana wote wanafanana kwa vitu wanavyohitaji lakini cha msingi ni kujua how women act, think and feel when they are in love. Zifuatazo ni vitu ambavyo msichana akifanyiwa ujisikia special.
(a)Wasichana wengi wanapenda utulivu
Hivi unajua ni kwa nini wasichana wengi hawapendi kwenda bar, na badala yake wanapendelea kenda parties ambapo wanaweza kukutana na watu wa aina mbalimbali. Ni makosa ya wanaume wengi kwani wao ufikiri kuwa bar ni sehemu nzuri ya kukutana na mwanamke (hapa ndugu zangu wanywaji mnisamehe). 
 
Ukweli ni kwamba wanawake wengi hupenda kujikita kwenye vitu ambavyo vitakuza vipaji vyao, vitaongeza thamani yao katika jamii, kwa hiyo kama msichana anapenda movies basi mpeleke sehemu wanazoonesha sinema na kama anapenda pombe basi mpeleke bar (hapa ngugu zangu walevi tugonge cheers). Msichana siku zote hujisikia special ukimfanyia kitu anachokipenda na pia umweka huru zaidi.
(b) Je, vipi kuhusu wasichana wanaopata care nyingi kutoka kwa wanaume?
Kundi hili ni la wasichana ambao ni warembo kupita kiasi na kutokana na uzuri wao wameshazoea kufanyiwa vitu ambavyo vinawapa utulivu. Sasa hapa ni tofauti kidogo, kama unataka kumfanya ajisikie special msichana wa namna hii try to treat her as normally as possible, kwa sababu utakapo mpeleka sehemu alizozoea kupelekwa au utakapomfanyia vitu alivyozoea kufanyiwa sana kimoyomoyo atajisemeha huyu nae ni walewale hana jipya. 
Kwa hiyo kwa sampo hii jitahidi kwanza kumfanya ajisikie huru kwa mfano unawweza kumjengea mazingira kuwa unamwona kama dada yake, unamweshimu sana na pindi utakapokuwa nae jaribu kuwa fan and joking. Mchekeshe mfurahishe na ikiwezekana mtanie.
(c) Njia rahisi za kumfanya ajisikie special
Mwanaume hautaji kutumia mda na hela nyingi kumfanya msichana ajisikie special viyu vidogo vidpgo tu vinatosha kwa mfano unaweza kumtumia sms asubuhi, mchana na jioni hii inatosha kumfanya aone unamwaza kila wakati kwa hiyo yeye ni special. 
Pia unaweza kumuuliza kuhusu siku yake ilivyoeenda hii mara nyingi ni mda wa usiku kabla hajalala, hapa utapata nafasi ya kuanzisha mazungumzo mengine na pia atajua kuwa unayapenda maisha yake.Kitu kingine ambacho ni rahisi zaidi ila kina madhara kama hutokitilia maanani ni ‘promise’ keep your promise kwa kila kitu ulichokisema hapa atajisikia special.
(2)MFANYE AJISIKIE UNAMPENDA
Hapa niwaachie wasomaji, ebu niambie kwa mtazamo wako njia au vitu vya kufanya ili mwanamke ajione unampenda.... kazi kwenu ila msisahau kipimo cha ulijali hakipimwi kwa kulala na wanawake wengi la hasha manhood is measured by how well a man can love a women.

0 comments:

Chapisha Maoni