JINSI YA KUFANYA ILI KURUDIANA NA MPENZI WAKO WA ZAMANI-3
Leo
tunaendelea na hatua ya 4 na ya mwisho katika muendelezo wa njia au jinsi ya
kufanya kurudiana na mpenzi wako wa zamani. Kupata hatua za mwanzo bofya http://eliasadolf.blogspot.com au
kwenye facebook page inayoitwa eliado love stories.
HATUA YA 4: WASILIANA NAE.
Kumbukuka
mpenzi wako alipokuacha, alikuona na kukuchukulia wewe ni mkosaji, mdhaifu na
usiyejiheshimu. Lakini kwa kitendo chako cha kumtomtafuta kwa mda, lazima
ashangae na kujiuliza maswali mengi juu yako. Je, amepata mwingine mzuri zaidi
yangu? Je hanipendi tena?........
Hapa ataanza kusahau madhaifu yako yote na
kuanza kukukumbuka vitu vizuri ambavyo ulikuwa ukimfanyia. Ataanza kukumbuka
vitu vizuri ulivyo navyo wewe. Pindi utakapowasiliana nae, hakikisha unaongea
nae na ikibidi mnaonana. Vifuatavyo ni vitu vya kuzingatia kabla ujawasiliana
nae.
- Umehakikisha hujawasiliana nae zaidi ya mwezi
- Umefanya mabadiliko katika maisha yako
- Una uhakika kuwa kurudiana nae ni uamuzi sahihi
- Umekubaliana na sababu za nyie kuachana
- Una uhakika kuwa hata kama hatokubali kurudiana na wewe utaendelea na maisha yako ya furaha.
NJIA ZA KUWASILIANA NAE
(a) Barua pepe
Kwa
kuwa barua imepitwa na wakati katika kizazi hichi cha digital, unaweza kutumia
barua pepe au mitandao mingine ya kijamii. Barua pepe lazima iwe na malengo
matatu
- Kumfanya mpenzi wako aolewe kuwa umekubaliana na hali ya wewe na yeye kuachana. Na kwamba pia haikuwa kitu kibaya
- Kuomba msamaha sehemu zote ulizokosea
- Kumjulisha kuwa kuna mambo mazuri yanaendelea kukutokea katika maisha yako, mfano kupata kazi, kununua gari. Ila usimweleze sana ili awe na hamu ya kujua zaidi nini kimetokea kwenye maisha yako mara baada ya kuachana.
( (b) Ujumbe mfupi wa maneno
Sms
itume mara baada ya kutuma barua pepe.
Pia unaweza usitume barua ukatuma sms moja kwa moja, kwa sababu wewe ndo
unamjua zaidi mpenzi wako tumia njia yoyote ambayo utakayoona ni sahihi au zote
kwa pamoja.
Kitu
cha kuzingatia hapa unapowasiliana nae usizungumzie moja kwa moja kuhusu
uhusiano wenu. Pia epuka kutuma ujumbe usiojitosheleza. Ujumbe ambao utapunguza
yeye kujibu kitu kwa mfano
“mambo”
“i miss you” “upo” na zingine na kifupifupi.
Kamwe
usizungumzie kuhusu hisia na mapenzi au unataka kurudiana nae kwa mfano
“
i love you” “nateseka sana juu ya penzi lako” i want you back na zingine
unazozijua.
Epuka
kusema kitu kibaya kwenye meseji kama “ watoto wako wanakukumbuka sana,
ulifanya makosa sana kuwaacha wateseke” au “ kama usingekuwa na tamaa, naamini
tusingeachana”
Ila
unaweza kuandika vitu vifuatavyo katika ujumbe wako wa mneno
“
leo naangali filamu mpya ya Dimond na Wema, imenikumbusha pindi tukiwa pamoja.
Mkumbushe
vitu ambavyo mlishawahi kufanya pindi mlipokuwa pamoja kwa mfano
“
Dah, nimekumbuka siku tulivyokwenda Marangu waterfalls, siku ile ilikuwa ya furaha
sana. Nafurahi tulifurahia”au “Mambo, leo nimepika wali samaki nimekumbuka
jinsi ulivyokuwa ukinipikia”.
MUOMBE MUONANE
Baada
ya kuwasiliana nae muome muonane ana kwa ana, ila usimwambie kuwa ni siku ya
kufanya mapenzi, bali ni siku ya kuonana tu. Usimwoneshe kuwa unataka kurudiana
nae. Onesha kuwa unataka mtoke kama marafiki tu lakini unaweza kufanya vitu vya
kumvutia mnapokuwa pamoja.
Mfano kumkumbatia. Njia nzuri hapa ni kumkaribisha
chakuala au kuenda naekuanagalia sinema au sehemu yoyote yenye burudani.
Baada
ya hapo siku ingine lazinma takutafuta na kukuomaba muonane hapo usifanye
makosa na kuzungumzia mambo mabaya yaliyowafanya muachane, zaidi tazama mbele
anza upya.
Siku hii ni nzuri kama mtalimenya tunda na kukumbushia enzi zenu.
Amini sasa ni wako mpende kama zamani na sahau yaliyopiata wazungu wanasema
“there is no point digging old graves when you want to start a new life”....
KWA LEO TIUSHIE HAPA, ILA USIKOSE TOLEO LIJALO LINALOHUSU VITU VYA
KUFANYA ILI USIACHANE NA MPENZI WAKO.
0 comments:
Chapisha Maoni