Jumatatu, 3 Novemba 2014

DARASA HURU



ZIFAHAMU FAIDA NA HASARA ZA KAHAWA NA CHAI.
Watu wengi wamekuwa wakibishana  kipi bora kunywa kati ya kahawa na chai? Watumiaji wa vinywaji hivi kila mmoja amekuwa akieleza umuhimu wa kinywaji anachokipenda. Lakini kiukweli vyote kwa pamoja vina faida na hasara. Vinywaji hivi viwili vyote vinaweza kuongeza vitamini na kusaidia ubongo. 

Pamoja na faida nyingi za vinywaji hivi lakini wanywaji wanashauriwa kunywa kwa kiasi kwa sababu vyote vina Coffeine anaonya DR Jane Scearce. Ni dhairi kuwa kuna mgongano wa fikra juu ya faida na hasara za vinywaji mbalimbali. Zipo tafiti zinazosema Kahawa na chai zina faida na wapo wanaosema zina hasara.
ZIFUATAZO NI FAIDA ZA CHAI.
Kuna aina nyingi za chai ambazo ushawahi kuzisikia baadhi yake ni nzuri na baadhi yake ni mbaya. Ufati unaonesha kuwa aina yoyote ya chai inaongeza na kusaidia kufanya kazi kwa homoni inayoitwa Insulini mara kumi na tano zaidi.
Chai ya kijani inaaminika kuwa na kitu kinachoitwa kitaalam Antiozidants ambacho ni muhimu katika kuzuia saratani ya matiti, mapafu na tumbo. Pia chai ya kijani inasaidia kuzuia kuzuia magonjwa yanayoshambulia moyo na kupunguza uwezekano wa kupata presha. Wataalam pia wanaeleza kuwa chai ya kijani pia inasidia kuunguza fati na kuyeyusha mafuta yaliyoganda mwilini. 

Chai nyeusi ambayo mara nyingi inatengenezwa na majani yaliyokauka na hpitia kiwandani na huwa na kiwango kikubwa cha coffeine. Chai hii ni nzuri kwani inasaidia msukumo wa damu huyo hivyo kukulinda kutopata magonjwa ya moyo na mshtuko. Pia wataalam wanasema chai ya aina hii inasaidia mapafu kwa wale wanaovuta sigara.
Wataalam wanasema pia aina nyingine za chai kama chai nyeupe inasidia kupunguza uzito na pia zinasidia kulinda meno yasioze.

ZIFUATAZO NI FAIDA ZA KAHAWA.
Mara nyingi watu wamekuwa wakiogopakunywa kahawa kwa madai kuwa kahawa inaleta magonjwa ya moyo na saratani ya tumbo. Lakini ukweli ni kwamba maneno hayo hayana mantiki kama utakunywa kwa kiwango staili.
Kahawa inasidia kuongeza kumbukumbu na kupambana na magonjwa yanayoshambulia moyo. Pia kahawa inapunguza uwezekana wa kupata saratani ya matiti na utumbo mkubwa. Wataalam wanaeleza kuwa kahawa inasaidia kuongeza kuupa mwili nguvu.
Ila kunywa kahawa kwa wingi sio vizuri kwa afya yako anasema DR Jane Scearce. Inaweza kusababisha kutopata usingizi na macho kuwa mekundu.
Waatalam wanashauri wanashauri unywe mc 400 kwa mwanaume na 300mc kwa mwanamke, ambayo ni sawa na vikombe 4 kwa mwanaume na 3 kwa mwanamke. Lakini kwa upande wa chai ni vikombe 6 kwa mwanaume na 4 kwa mwamke.
Coffeine inatoa faida nyingi za kiafya ikiwa na pamoja na kupunguza maumivu, uchovu na kukufanya kazi kwa mda mrefu. Pia inasaidia misuli kutoshikamana wakati wa mazoezi ya mwili.
Mwisho ingawa ingawa kuna faida nyingi za kunywa chai na kahawa sio vizuri kunywa kupita kiasi. Kunywa kwa kiwango kidogo kinachopendekezwa na wataalam kwa siku.
USIKOSE DARASA HURU LA KESHO.


0 comments:

Chapisha Maoni