HATUA ZA KUFUATA KURUDIANA NA MPENZI WAKO WA ZAMANI-2.
Ndugu
wasomaji wa makala zangu za uhusiano leo tunaendelea na hatua za kufuata ili
kuweza kurudiana na mpenzi wako wa zamani. Hataua ya kwanza nilizungumzia
makosa ya kuepuka ukitaka kurudiana na mpenzi wako ikiwa ni pamoja na;
( (a)
kumpigia
simu au kutuma sms kila mara
( (b)
Kamwe
usimwombe msamaha.
(c) Usikubali kila kitu anachotaka
(d) Usiendelee kuonesha kuwa unamjali
(e) Usichukie ukigundua yupo na mtu
mwingine.
Kama ulikua hujasoma hatua ya kwanza, basi isome kwenye blog hii kupata mtiririko mzuri.
Leo tuendelee na na hatua ya pili na ya
tatu.
HATUA YA 2: USIWASILIANE NAE, JIPE MDA NA NAFASI.
Kuna
kitu kinachoitwa ‘no contact rule’ kwa lugha ya wenzetu. Kanuni hii ni rahisi
sana na inafanya kazi na yenye mafanikio makubwa. Kitu unachotakiwa kufanya ni
kuacha kuwasiliana na mpenzi wako wa zamani kwa mda. Hapa na maana kwamba
usimpigie. Kumtumia sms, kuchati nae twiter, facebook,whatsaap na mitandao
mingine ya kijamii. Ukiweza futa namba zake kabisa na pia epuka kwenda sehemu
ambazo mtaonana.
KWA NINI NISIWASILIANAE NAE?
( (a) Mpenzi
wako wa zamani anahitaji mda na nafasi kusahau maumivu yote baada ya kuachana,
na hii itamfanya aanze kukumbuka. Watu wengi wanafikiri kwamba eti kama usipo
wasiliana nae atakusahau kabisa, la hasha usipo wasiliana nae unampa mda wa
kukumbuka wewe na atakuwa anajiuliza kwa nini haumtafuti?.
Hapa unatakiwa
ukumbuke yale makosa niliyokuzuia kuyafanya katika hatua ya kwanza. Kitendo
chako cha kutomtafuta kinakufanya usionekane mdhaifu bali ngangari na usiye na
uhitaji mkubwa.
(c) Lazima
uwe mtu mwenye furaha kwa kipindi hiki cha mpito.
Unaitaji kuyathamini maisha
yako kwa sasa. Hii itakusaidia pindi utakapokutana na mpenzi wako baada ya “no contact period”
avutiwe na wewe na kuona kuwa wewe ni mtu mpya.
NISIWASILIANE NAE KWA MDA GANI?
Kwa
kawaida usiwasiliane nae mpaka pale utakapojiona kuwa umebadilisha maisha yako
na unaweza kuendelea hata bila yeye. Kitaalam siku 30 zizatosha lakini unaweza
kuchukua hata miezi 2 au 6 kutegemea na sababu zilizowafanya muachane.
Kitu cha
muhimu hapa kwa kipindi hiki usije ukamwambia kuwa naacha kuwasiliana na wewe
kwa mda fulani. Kitendo cha kutowasiliana nae sio ukatili bali ni kwa ajili ya
afya ya akili na mwili wako. Kipindi hiki pia usipokee simu zake wala kujibu
sms zake.
Sehemu hii ni muhimu zaidi ndugu yangu ni muhimu sana ndugu yangu. No contact(kutokuwasiliana) hakutakuwa na maana mpaka hapo utakapoamua kubadilsha maisha yako na kuwa bora zaidi. Jijali kwa;
( (a) Badilisha muonekano wako
na kuwa mzuri zaidi.
Badilisha muonekano wako, kimavazi
kutakufanya uonekane wa thamani zaidi. Unaweza kubadilisha jinsi ya uvaaji,
jinsi ya unyoaji ukawa wa kisasa zaidi na unayeendana na wakati. Unaweza
kutengeneza mwili wako kwa kufanya mazoezi na kwenda gym. Hapa kuwa makini
kidogo usije ukafanya vitu visivyokubalika miongoni mwa jamii inayokuzunguka au
ukafanya kitu ambacho uwezi kukisahau kama kuchora tatuu.
( (b)
Badilisha fikra zako na
mawazo yako.
Kuwa
mtu mwenye furaha na mwenye kujiamini ni jambo ambalo litakusaidia kurudiana na
mpenzi wako. Mpenzi msomaji lazima utambue kuwa furaha ni kitu cha pekee
ambachi kinatoka moyoni mwako na akilini pia. Vitu vinavyoweza kukupa furaha ni
pamoja na kutoka out na marfiki zako, tembelea kumbi za starehe kama kuangalia
sinema, kusoma vitabu vya ujasiria mali na kadhalika.
KWA LEO TUISHIE HAPA USIKOSE HATUA YA NNE.
0 comments:
Chapisha Maoni