HATUA ZA KUFUATA KURUDIANA NA MPENZI
WAKO WA ZAMANI.
Ndugu wapendwa wasomaji wa makala zangu za na wasalimu
kwa kusema amani itawale. Leo katika lovezone nawaletea darasa mahususi kuhusu
mbinu unazoweza kurudiana na mpenzi wako wa zamani ambaye bado unampenda.
Unajua kuna sababu nyingi zinazofanya watu waachane ilihali bado wanapendana.
Siku ingine tutazungumzia sababu hizo ila leo ngoja tuende moja kwa moja kwenye
mada.
Unajua kurudiana na mpezi wako wa zamani sio
ishara kuwa wewe ni limbukeni au hakuna zaidi yake bali siku zote ni vizuri
kuheshimu hisia zako. Kama bado unampenda na unahisi yeye ni furaha yako sasa
kwa nini msirudianae? Labda nikwambie kurudiana na mpenzi wako sio kazi ngumu,
kazi ngumu ni kuhakikisha kuwa hamuachani tena. Ebu fikiria kama mtu akiweza
kukuacha, utawezaje kurudiana nae na kumfanya hasikuache tena? Kuna umuhimu
gani wa kurudiana nae kama mtaweza kuachana tena.
Kuna njia za kufuata ili uweze kurudiana na
mpenzi wako wa zamani, kwa sababu pindi tu ulipoachana nae uliumia sana,
ulipoteza hisia juu yake na kubwa zaidi ulichanganyikiwa. Na kwa kawaida katika
kupindi hichi cha mafarakano, kuna nafasi kubwa ya kufanya makosa ambayo
yatakufanaya ushindwe kurudiana na mpenzi wako wa zamani. Katika hatua nne za
kufuata ili kurudiana na mpenzi wako wa zamani. Hatua ya kwanza inaeleza makosa
ambayo ni muhimu kuyaepuka ili uweze kurudiana na mtu ambaye bado unampenda.
HATUA YA 1. EPUKA MAKOSA HAYA.
(a)
kumpigia simu au kutuma sms kila mara
Ni kosa kubwa sana kumtumia meseji au kumpigia
simu mpenzi wako pindi tu mnapoachana. Watu wengi wanafikiri kwamba kuendelea
kuwasiliana na Ex wako kutamfanya asikusahau na kukusamehe lakini kitaalam njia
hiyo sio sahihi. Unajua unapompigipigia simu na kuwasiliana nae hii ina
maanisha kuwa hujiamini na bila yeye huwezi kuishi. Kumwonesha kuwa umamwitaji
sana na unateseka bila uwepo wake huwezi kuishi kumtamfanya azidi kuwa mbali na
wewe. Hapa kwa wale rafiki zangu wanaotumia vilevi lazima wawe makini sana hasa
wanapokunywa pombe na kulewa kupita kiasi hii ni kwa sababu mara nyingi
wanapolewa hujikuta wakiwapigia simu ex wao na kitendo hicho huwafanya
waonekane wapuuzi zaidi. Najua watu wengi watauliza sasa Eliado nisipompigia
wala kumtumia meseji ni vipi ntaweza kurudiana nae? Kuna jinsi ya kuwasiliana
nae ambapo utamfanya avutiwe na wewe tena. Ntaeleza jinsi ya kuwasiliana nae
katika hatua ya 4.
(b)
Kamwe usimwombe msamaha.
Kama msamahaa una maana baada ya kuachana au
ni suluhisho basi hakuna watu ambao wangeachana duniani. Unajua mtu akikuacha
siku zote anajua utamwomba msamaha. Sababau yoyote iliyowafanya muachane
haitobadilishwa kwa kitendo chako cha kuomba msamaha. Kitu cha pekee msamaha
kitakusaidia ni kuendelea kuonekana dhaifu na mtu usiyejiweza. Na siku zote
tambua ya kuwa hakuwa msichana au mvulana anayependa kuendelea kuwa na mtu
dhaifu. Watu wengi wanfikiri kwa kitendo cha kumwambia msichana wako au mvulana
kuwa huwezi kuishi bila yeye kitasaidia
kumrudisha la hasha utazidi kumpoteza kabisa. Najua hatua hii ni ngumu lakini
utanielea tu ndugu yangu.
(c)
Usikubali kila kitu anachotaka
Watu
wengi wanafikiri kuwa eti ukimkubalia kila kitu anachotaka atarudiana na wewe.
Kwamba vitu vyote vyote si kitu, bali kitu cha muhimu ni kurudiana nae kwa
gharama yoyote ile, huo ni upuuzi ndugu yangu. Kuwa tayari kwa lolote hakuta
kusaidia kurudiana na mpenzi wako zaidi ya kumfanya akuzarau na kukuona dhaifu
sana. Narudia tena ndugu msomaji hakuna mtu anayependa kuwa na mahusiano na
mvulana au msichana dhaifu.
(d)
Usiendelee
kuonesha kuwa unamjali
Najua wengi wanafikiri kuwa eti ukionesha
jinsi gani bado unampenda na kumjali mtarudiana. Pia wengine wanajisumbua
kumwonesha mtu aliyeachana naye kuwa hakuna mtu mwingine duniani anaweza
kumpenda jinsi anavyompenda yeye. Ukweli ni kwamba mtu uliyekuwa naye anajua
jinsi gani unavyompenda, kumjali na kumuheshimu lakini bado alikuacha. Ki
ukweli kumwonesha kumjali hakutakusaidia kwa sasa zaidi ya kumfanya akuchukie
zaidi ya kumfanya akuchukie zaidi.
(e)
Usichukie ukigundua yupo na mtu mwingine.
Ni ukweli usiopingika kwamba watu wengi
wanaumia sana wanapogundua kuwa mpenzi wake wa zamani anatoka na mtu mwingine.
Watu wengi hali hii uwaumiza na kujisemea “kama nisipofanya kitu sasa mtu wangu
atazama kwenye mapenzi na mtu mwingine. Hapa ndipo watu wengi wanfanya makosa
niliyoyaeleza hapo juu kama kuomba msamaha, kumwambia ni kiasi gani bado
anampenda au kukubali masharti yote atakayopewa.
Bado
watu wengine uenda mbali zaidi na kujikuta unampigia simu na kumtumia sms siku
nzima. Mbaya zaidi utakuta mtu anaamua kumchafua mtu ambaye anatoka na mpenzi
wako wa zamani. Haya ni makosa makubwa cha msingi ndugu yangu jua kuwa kama
mpenzi wako alikupenda kwa dhati na mahusianao yenu yalikuwa ya maana na yenye
nguvu basi mahusiano atakayoanzisha yatakuwa ni ya mda mfupi tu.
Ni
ukweli usiopingika kuwa kuingia kwenye mahusiano mapya ni njia watu wengi
utumia kukabiliana na breakup(kuachana). Njia hii ni ya zima moto na kama
mlipendana, hawezi kukusahau na lazima atapenda kurudiana na wewe siku moja.
Kitu muhimu ni kutulia tu pindi mtu wako
anapojaribu kutoka na mtu mwingine. Kwa vyovyote vile husimwambie mpenzi wako
aachane na mtu aliyenaye kwa sasa. Ukweli ni kwamba atayeye moyoni mwake
atakuwa na kidonda cha kuachana hivyo kuwa na mtu mwingine hakiwezi pona kwa
urahisi.
Nafasi bado ipo hata kama tayari ulishafanya
baadhi ya makosa niliyoyataja baada ya kuachana. Usijali na kuumia sana kwani
hata wataalamu wa saikolojia, matajiri na maprofesa uishia kufanya makosa hayo
baada ya mfarakano.
Ni kawaida kwa mwanadamu kukosea na waswahi li usema
tutajifunza kutokana na makosa. Kitu cha muhimu ni kujua kuwa makosa haya
hayatakusaidia kurudiana na mpenzi wako na ukiweza acha kuyafanya.
Kwa leo tuishie hapa, Next time tutaendela na
hatua ya 2,3 na 4.
0 comments:
Chapisha Maoni