KWA NINI WANAUME WENYE SURA MBAYA WANAMILIKI WASICHANA WAREMBO.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhg76yzsRH5gOSwlN705EdYjHvX6xwqcOEnKeYCsGlIvo_1R-5D82msVXxyRkN_SenUQ9KJyWXb7geSrV-HSep_eNM240X1guxh0LB_vZYQrm_UMbpEetKt4v5y6VzcBinwcEjn7AAgpBM/s1600/ugly_dudehotchick.jpg)
Hivi ushawahi kujiuliza kwa nini baadhi ya wanaume wenye sura mbaya wanamilki wasichana warembo hapa mjini? Je, ni kweli kwamba wanawake warembo wanavutiwa na wanaume wenye sura mbaya au washambashamba? Kama sivyo, je ni kitu gani cha ziada wanawake wenye mvuto hupenda kutoka kwa wanaume wa namna hii?
Hivi hushangai kuona mwanaume ambaye
hana mvuto anakuwa na msichana mrembo, tena utamkuta mvulana kama huyo
yupo kwenye mahusiano mazuri ya kimapeenzi na wewe na u handsomeboy wako
upo singe na wasichana warembo wanakukimbia.
Je, ni kitu gani watu wa namna hii wanakuwa nacho na wewe huna? Jibu ni rahisi sana mpendwa msomaji, kwanza wanaume wenye sura mbaya wenyewe hawajifikirii kuwa hawana mvuto, tena isitoshe wao huwa hawafikirii muonekano wao mbele ya wasichana warembo, wao hujiona wapo poa tu na wakati mwingine wanajivunia kuwa wakipekee.
Je, ni kitu gani watu wa namna hii wanakuwa nacho na wewe huna? Jibu ni rahisi sana mpendwa msomaji, kwanza wanaume wenye sura mbaya wenyewe hawajifikirii kuwa hawana mvuto, tena isitoshe wao huwa hawafikirii muonekano wao mbele ya wasichana warembo, wao hujiona wapo poa tu na wakati mwingine wanajivunia kuwa wakipekee.
Hali hiyo ya kujikubali huwafanya wawe
wanavaa jinsi wanavyojisikia na kulingana na uwezo wao, hivyo huwa
comfortable wanapokutana na wasichana warembo. Sasa wewe unayejifanya
handsomeboy utaendelea kusubiri kwa kuwa kila kukicha unawaza uvae nini.
Wanaume ambaye huwa anafikiria kuwa yeye hana mvuto kulinganisha na watu wengine maarufu huwa anajimaliza mwenyewe kisaikolojia na hii umjengea mazingira ya uwoga pindi anapokutana na msichana mrembo.
Wanaume ambao hawajiamini hutumia nguvu nyingi kufikiria jinsi alivyo
badala ya kutumia nguvu hizo kujenga mahusiano na wasichana warembo.
Wavulana wasio na mvuto hawatumii mda mwingi kujifikiria na hata
wanapotoka out na wasichana huwa kama ni vichekesho kitu ambacho kina
create attention kwa wasichana kuenjoy uwepo wao.
Kwa hiyo kitu pekee ambacho ugly guys wanacho ni kujiamini, mvulana hasiyejiamini mara nyingi anajiuliza uliza maswali hivi kweli na mimi na stahili kuwa na msichana mrembo kama yule? Maswali haya huwafanya washindwe kujieleza pindi wanapokutana na wasichana warembo. Wasichana siku zote hawapendi wanaume wasiojiamini.
Kwa nini kujiamini ni silaa zidi ya wasichana warembo? Jibu ni rahisi kwanza lazima tukubaliane kuwa wasichana warembo huwa wanatongozwa mara nyingi na mara nyingi wanaume wanaowatokea ni wale wanaojiamini ni ma handsomeboy na kwa kawaida ya wanume hawa hujaribu kujionesha kuwa wao ni watu wazuri na wenye uwezo wa kuwamiliki.
Sasa kwa kuwa kila siku msichana mrembo anatongozwa na
wanaume wa namna hii basi kwao huwa ni mazoea ukienda na staili hiyo
hawaoni jipya kwa kuwa ata jana aliambiwa hivyo hivyo. Wasichana warembo
wanataka kitu cha pekee ambacho hawajawahi kuambiwa, kusikia au kuona,
wanataka wakutane na mwanaume anayejiamini sio mwoga na pia ambaye
anajikubali jinsi alivyo hata kama ni mbaya kiasi gani.
Kujiamini ni silaa kubwa kwa mwanaume anayetaka kumiliki msichana mrembo. Ila kujiamini tu haitoshi mwanaume anatakiwa awe mcheshi, mchangamfu na mkweli vitu ambavyo vitampa nafasi ya kusikilizwa pindi anapokutana na msichana mrembo.
KWA LEO TUISHIE HAPA. ENDELEA KUFUATILIA BLOG HII UPATE BURUDANI NA MAFUNZO.
0 comments:
Chapisha Maoni