Jumanne, 4 Novemba 2014

UHUSIANO



JINSI YA KUFANYA ILI KURUDIANA NA MPENZI WAKO WA ZAMANI-3

Leo tunaendelea na hatua ya 4 na ya mwisho katika muendelezo wa njia au jinsi ya kufanya kurudiana na mpenzi wako wa zamani. Kupata hatua za mwanzo bofya http://eliasadolf.blogspot.com au kwenye facebook page inayoitwa eliado love stories.
HATUA YA 4: WASILIANA NAE.
Kumbukuka mpenzi wako alipokuacha, alikuona na kukuchukulia wewe ni mkosaji, mdhaifu na usiyejiheshimu. Lakini kwa kitendo chako cha kumtomtafuta kwa mda, lazima ashangae na kujiuliza maswali mengi juu yako. Je, amepata mwingine mzuri zaidi yangu? Je hanipendi tena?........ 
Hapa ataanza kusahau madhaifu yako yote na kuanza kukukumbuka vitu vizuri ambavyo ulikuwa ukimfanyia. Ataanza kukumbuka vitu vizuri ulivyo navyo wewe. Pindi utakapowasiliana nae, hakikisha unaongea nae na ikibidi mnaonana. Vifuatavyo ni vitu vya kuzingatia kabla ujawasiliana nae.

  1. Umehakikisha hujawasiliana nae zaidi ya mwezi  
  2. Umefanya mabadiliko katika maisha yako
  3. Una uhakika kuwa kurudiana nae ni uamuzi sahihi 
  4. Umekubaliana na sababu za nyie kuachana
  5. Una uhakika kuwa hata kama hatokubali kurudiana na wewe utaendelea na maisha yako ya furaha.
NJIA ZA KUWASILIANA NAE
(a)    Barua pepe
Kwa kuwa barua imepitwa na wakati katika kizazi hichi cha digital, unaweza kutumia barua pepe au mitandao mingine ya kijamii. Barua pepe lazima iwe na malengo matatu
  1. Kumfanya mpenzi wako aolewe kuwa umekubaliana na hali ya wewe na yeye kuachana. Na kwamba pia haikuwa kitu kibaya
  2.   Kuomba msamaha sehemu zote ulizokosea
  3.   Kumjulisha kuwa kuna mambo mazuri yanaendelea kukutokea katika maisha yako, mfano kupata kazi, kununua gari. Ila usimweleze sana ili awe na hamu ya kujua zaidi nini kimetokea kwenye maisha yako mara baada ya kuachana.
(     (b)   Ujumbe mfupi wa maneno
Sms itume  mara baada ya kutuma barua pepe. Pia unaweza usitume barua ukatuma sms moja kwa moja, kwa sababu wewe ndo unamjua zaidi mpenzi wako tumia njia yoyote ambayo utakayoona ni sahihi au zote kwa pamoja.
Kitu cha kuzingatia hapa unapowasiliana nae usizungumzie moja kwa moja kuhusu uhusiano wenu. Pia epuka kutuma ujumbe usiojitosheleza. Ujumbe ambao utapunguza yeye kujibu kitu kwa mfano
“mambo” “i miss you” “upo” na zingine na kifupifupi.
Kamwe usizungumzie kuhusu hisia na mapenzi au unataka kurudiana nae kwa mfano
“ i love you” “nateseka sana juu ya penzi lako” i want you back na zingine unazozijua.
Epuka kusema kitu kibaya kwenye meseji kama “ watoto wako wanakukumbuka sana, ulifanya makosa sana kuwaacha wateseke” au “ kama usingekuwa na tamaa, naamini tusingeachana”
Ila unaweza kuandika vitu vifuatavyo katika ujumbe wako wa mneno
“ leo naangali filamu mpya ya Dimond na Wema, imenikumbusha pindi tukiwa pamoja.
Mkumbushe vitu ambavyo mlishawahi kufanya pindi mlipokuwa pamoja kwa mfano
“ Dah, nimekumbuka siku tulivyokwenda Marangu waterfalls, siku ile ilikuwa ya furaha sana. Nafurahi tulifurahia”au “Mambo, leo nimepika wali samaki nimekumbuka jinsi ulivyokuwa ukinipikia”.
MUOMBE MUONANE
Baada ya kuwasiliana nae muome muonane ana kwa ana, ila usimwambie kuwa ni siku ya kufanya mapenzi, bali ni siku ya kuonana tu. Usimwoneshe kuwa unataka kurudiana nae. Onesha kuwa unataka mtoke kama marafiki tu lakini unaweza kufanya vitu vya kumvutia mnapokuwa pamoja. 
Mfano kumkumbatia. Njia nzuri hapa ni kumkaribisha chakuala au kuenda naekuanagalia sinema au sehemu yoyote yenye burudani.
Baada ya hapo siku ingine lazinma takutafuta na kukuomaba muonane hapo usifanye makosa na kuzungumzia mambo mabaya yaliyowafanya muachane, zaidi tazama mbele anza upya. 
Siku hii ni nzuri kama mtalimenya tunda na kukumbushia enzi zenu. Amini sasa ni wako mpende kama zamani na sahau yaliyopiata wazungu wanasema “there is no point digging old graves when you want  to start a new life”....
KWA LEO TIUSHIE HAPA, ILA USIKOSE TOLEO LIJALO LINALOHUSU VITU VYA KUFANYA ILI USIACHANE NA MPENZI WAKO.

Jumatatu, 3 Novemba 2014

DARASA HURU



ZIFAHAMU FAIDA NA HASARA ZA KAHAWA NA CHAI.
Watu wengi wamekuwa wakibishana  kipi bora kunywa kati ya kahawa na chai? Watumiaji wa vinywaji hivi kila mmoja amekuwa akieleza umuhimu wa kinywaji anachokipenda. Lakini kiukweli vyote kwa pamoja vina faida na hasara. Vinywaji hivi viwili vyote vinaweza kuongeza vitamini na kusaidia ubongo. 

Pamoja na faida nyingi za vinywaji hivi lakini wanywaji wanashauriwa kunywa kwa kiasi kwa sababu vyote vina Coffeine anaonya DR Jane Scearce. Ni dhairi kuwa kuna mgongano wa fikra juu ya faida na hasara za vinywaji mbalimbali. Zipo tafiti zinazosema Kahawa na chai zina faida na wapo wanaosema zina hasara.
ZIFUATAZO NI FAIDA ZA CHAI.
Kuna aina nyingi za chai ambazo ushawahi kuzisikia baadhi yake ni nzuri na baadhi yake ni mbaya. Ufati unaonesha kuwa aina yoyote ya chai inaongeza na kusaidia kufanya kazi kwa homoni inayoitwa Insulini mara kumi na tano zaidi.
Chai ya kijani inaaminika kuwa na kitu kinachoitwa kitaalam Antiozidants ambacho ni muhimu katika kuzuia saratani ya matiti, mapafu na tumbo. Pia chai ya kijani inasaidia kuzuia kuzuia magonjwa yanayoshambulia moyo na kupunguza uwezekano wa kupata presha. Wataalam pia wanaeleza kuwa chai ya kijani pia inasidia kuunguza fati na kuyeyusha mafuta yaliyoganda mwilini. 

Chai nyeusi ambayo mara nyingi inatengenezwa na majani yaliyokauka na hpitia kiwandani na huwa na kiwango kikubwa cha coffeine. Chai hii ni nzuri kwani inasaidia msukumo wa damu huyo hivyo kukulinda kutopata magonjwa ya moyo na mshtuko. Pia wataalam wanasema chai ya aina hii inasaidia mapafu kwa wale wanaovuta sigara.
Wataalam wanasema pia aina nyingine za chai kama chai nyeupe inasidia kupunguza uzito na pia zinasidia kulinda meno yasioze.

ZIFUATAZO NI FAIDA ZA KAHAWA.
Mara nyingi watu wamekuwa wakiogopakunywa kahawa kwa madai kuwa kahawa inaleta magonjwa ya moyo na saratani ya tumbo. Lakini ukweli ni kwamba maneno hayo hayana mantiki kama utakunywa kwa kiwango staili.
Kahawa inasidia kuongeza kumbukumbu na kupambana na magonjwa yanayoshambulia moyo. Pia kahawa inapunguza uwezekana wa kupata saratani ya matiti na utumbo mkubwa. Wataalam wanaeleza kuwa kahawa inasaidia kuongeza kuupa mwili nguvu.
Ila kunywa kahawa kwa wingi sio vizuri kwa afya yako anasema DR Jane Scearce. Inaweza kusababisha kutopata usingizi na macho kuwa mekundu.
Waatalam wanashauri wanashauri unywe mc 400 kwa mwanaume na 300mc kwa mwanamke, ambayo ni sawa na vikombe 4 kwa mwanaume na 3 kwa mwanamke. Lakini kwa upande wa chai ni vikombe 6 kwa mwanaume na 4 kwa mwamke.
Coffeine inatoa faida nyingi za kiafya ikiwa na pamoja na kupunguza maumivu, uchovu na kukufanya kazi kwa mda mrefu. Pia inasaidia misuli kutoshikamana wakati wa mazoezi ya mwili.
Mwisho ingawa ingawa kuna faida nyingi za kunywa chai na kahawa sio vizuri kunywa kupita kiasi. Kunywa kwa kiwango kidogo kinachopendekezwa na wataalam kwa siku.
USIKOSE DARASA HURU LA KESHO.


Jumapili, 2 Novemba 2014

UHUSIANO



HATUA ZA KUFUATA KURUDIANA NA MPENZI WAKO WA ZAMANI-2.

 
Ndugu wasomaji wa makala zangu za uhusiano leo tunaendelea na hatua za kufuata ili kuweza kurudiana na mpenzi wako wa zamani. Hataua ya kwanza nilizungumzia makosa ya kuepuka ukitaka kurudiana na mpenzi wako ikiwa ni pamoja na;
(       (a)   kumpigia simu au kutuma sms kila mara
(       (b)   Kamwe usimwombe msamaha.
(c)  Usikubali kila kitu anachotaka
(d)   Usiendelee kuonesha kuwa unamjali
(e)   Usichukie ukigundua yupo na mtu mwingine.

Kama ulikua hujasoma hatua ya kwanza, basi isome kwenye blog hii kupata mtiririko mzuri.

Leo tuendelee na na hatua ya pili na ya tatu.
HATUA YA 2: USIWASILIANE NAE, JIPE MDA NA NAFASI.
Kuna kitu kinachoitwa ‘no contact rule’ kwa lugha ya wenzetu. Kanuni hii ni rahisi sana na inafanya kazi na yenye mafanikio makubwa. Kitu unachotakiwa kufanya ni kuacha kuwasiliana na mpenzi wako wa zamani kwa mda. Hapa na maana kwamba usimpigie. Kumtumia sms, kuchati nae twiter, facebook,whatsaap na mitandao mingine ya kijamii. Ukiweza futa namba zake kabisa na pia epuka kwenda sehemu ambazo mtaonana.
KWA NINI NISIWASILIANAE NAE?
(    (a) Mpenzi wako wa zamani anahitaji mda na nafasi kusahau maumivu yote baada ya kuachana, na hii itamfanya aanze kukumbuka. Watu wengi wanafikiri kwamba eti kama usipo wasiliana nae atakusahau kabisa, la hasha usipo wasiliana nae unampa mda wa kukumbuka wewe na atakuwa anajiuliza kwa nini haumtafuti?. 
  Hapa unatakiwa ukumbuke yale makosa niliyokuzuia kuyafanya katika hatua ya kwanza. Kitendo chako cha kutomtafuta kinakufanya usionekane mdhaifu bali ngangari na usiye na uhitaji mkubwa.

    (b) Wewe pia unahitaji mda na nafasi, kujitafakari na kujua wapi ulikosea. Unaitaji mda kutafakari kama kuna ulazima wa kurudiana na mtu aliyekuacha au la?Unaitaji kujifunza kama unaweza kuishi bila yeye. Unaitaji mda kujirizisha kuwa unaweza  kuishi ukiwa na furaha bila yeye.Ni kukumbushe kuna msemo usemao “Furaha haiji kwa kupata kitu ambacho huna bali kwa kukipenda kitu ulichonacho. 
(c) Lazima uwe mtu mwenye furaha kwa kipindi hiki cha mpito.
Unaitaji kuyathamini maisha yako kwa sasa. Hii itakusaidia pindi utakapokutana na  mpenzi wako baada ya “no contact period” avutiwe na wewe na kuona kuwa wewe ni mtu mpya.
 NISIWASILIANE NAE KWA MDA GANI? 
Kwa kawaida usiwasiliane nae mpaka pale utakapojiona kuwa umebadilisha maisha yako na unaweza kuendelea hata bila yeye. Kitaalam siku 30 zizatosha lakini unaweza kuchukua hata miezi 2 au 6 kutegemea na sababu zilizowafanya muachane.  
 Kitu cha muhimu hapa kwa kipindi hiki usije ukamwambia kuwa naacha kuwasiliana na wewe kwa mda fulani. Kitendo cha kutowasiliana nae sio ukatili bali ni kwa ajili ya afya ya akili na mwili wako. Kipindi hiki pia usipokee simu zake wala kujibu sms zake.

HATUA YA 3: JIJALI MWENYEWE
Sehemu hii ni muhimu zaidi ndugu yangu ni muhimu sana ndugu yangu. No contact(kutokuwasiliana) hakutakuwa na maana mpaka hapo utakapoamua kubadilsha maisha yako na kuwa bora zaidi. Jijali kwa;
(      (a) Badilisha muonekano wako na kuwa mzuri zaidi. 
   Badilisha muonekano wako, kimavazi kutakufanya uonekane wa thamani zaidi. Unaweza kubadilisha jinsi ya uvaaji, jinsi ya unyoaji ukawa wa kisasa zaidi na unayeendana na wakati. Unaweza kutengeneza mwili wako kwa kufanya mazoezi na kwenda gym. Hapa kuwa makini kidogo usije ukafanya vitu visivyokubalika miongoni mwa jamii inayokuzunguka au ukafanya kitu ambacho uwezi kukisahau kama kuchora tatuu.
(        (b)   Badilisha fikra zako na mawazo yako.
Kuwa mtu mwenye furaha na mwenye kujiamini ni jambo ambalo litakusaidia kurudiana na mpenzi wako. Mpenzi msomaji lazima utambue kuwa furaha ni kitu cha pekee ambachi kinatoka moyoni mwako na akilini pia. Vitu vinavyoweza kukupa furaha ni pamoja na kutoka out na marfiki zako, tembelea kumbi za starehe kama kuangalia sinema, kusoma vitabu vya ujasiria mali na kadhalika.
KWA LEO TUISHIE HAPA USIKOSE HATUA YA NNE.