EVERLASTING
LOVE. (Penzi la milele)
SEHEMU YA 5
MTUNZI: ELIAS ADOLF (eliado)
RACHAEL ANAPATA
MARAFIKI
Snoga ana marafiki wengi sana miongoni mwao ni Alex
Kijoji huyu ni rafiki yake kwanza wanakaa chemba moja, pili wanasoma kidato
kimoja mkondo mmoja na mwaka huo walikuwa form three. Alex yeye anatokea Kondoa
Dodoma lakini kwa sasa alikuwa anaishi Dar es salaaam kwa kaka yake. Kaka yake
huyo aliamua kumsomesha baada
ya baba yao mpendwa kufariki dunia.
Alex anatokea kuwa maarufu sana kwa kuwa
na matumizi makubwa sana ya fedha walimpachika jina la B.O.T, kundi lao hilo
liliundwa na na yeye pamoja na rafiki yake kipenzi Lucas huyu kweli alikuwa ana
hela kwani enzi hizo alikuwa anamiliki simu ya laki tano nae alitokea kondoa
japo kwao kabisa ni moshi na familia yao ilikuwa inamiliki mabasi yaendayoamikoani.
Siku moja Snoga na Alex waliamua kushuka huko
bondeni yaani bustanini kwa kina Rachael kwenda kuangaza angaza macho, ndipo
hapo wanaonana na Rachael na kupata upenyo wa kusalimiana kwani siku hiyo
wanafunzi hao walikuwa peke yao bila matron wao.
Snoga kama kawaida yake
alimtambulisha rafiki yake kwa Rachael akitia manjonjo mengi yasiyoitajika.
Rachael alifurahi sana kuonana na Alex kwani alitokea kuvutiwa sana na kaka
huyo tangia siku nyingi. kilichofuata hapo ni kupanga njia ya kumpata
mtanashati huyu lakini kazi ilikuwa ngumu kwani mtu ambaye hamjazoeana ni kazi
sana kumwingiza mtegoni. Shughuli ilianza kwani usiku kucha Rachael hakulala
kwa kumwazia Alex na hata alipopata usingizi bado alimwota tena ndoto pevu,
alipoamka picha ya Alex ilimjia machoni mwake, basi taratibu alijikuta akikosa
raha siku nzima.
Baada kama ya siku tatu Rachael akapatwa na ugonjwa wa
malaria, ingawa kiukweli haikuwa malaria bali msongo wa mawazo na akalazwa
katika dispensary iliyopo hapo hapo mission.
Snoga aliposikia Rachael amelazwa, aliamua kwenda
kumwona lakini safari hii hakuwa na ALEX alikuwa na rafiki yake mwingine,
Rachael alifurahi sana na kitu cha kwanza kuuliza ilikuwa rafiki yake yukwapi
yaani ALEX.
Snoga akamwambia nilimwacha ana shughuli nyingi pale shuleni kwani
siku hiyo ilikuwa ya usafi na yeye ni kiongozi tena wa afya hivyo alikuwa
anasimamia usafi. Rachael alikasirika moyoni ingawa hakuonesha usoni, wanafunzi
hawa wa Kwiro walipoaga kitu muhimu walichosisitizwa ni kwamba wasisahau
kumwambia Alex aende kumwona.
Snoga baada ya kufika shuleni alifikisha ujumbe
alopewa ingawa kwa shingo upande kwani alishaanza kuhisi kuna kitu kilikuwa
kimejificha haiwezekani watu wamejuana siku moja tu tena kwa mgongo wangu alafu
auliziwe hivyo. Ujue kwa uzuri wa Rachael kila mwananaume alitaka kuwa nae sasa
kilchomsumbua Snoga ni wivu na tamaa.
Siku iliyofuata Alex alikwenda kumsalimia Rachael
akajikuta bila kutegemea kwa mara yake ya kwanza maishani anabeba kadi ya pole,
soda, biscuit na matunda kwenye kilasketi chake ambacho huwa kinawachengua watu
hasa maduu pindi akivaapo. Alipooingia tu wodini Rachael aliinuka ghafla na
kukaa huku mapigo ya moyo wake yakiongezeka.
Alex alifanikiwa kuigundua hali
hiyo lakini hakushangaa sana, walipiga stori nyingi sana ikiwa ni pamoja na
kutambulishana vizuri. Rachael alijitambulisha kuwa yeye anatokea masaki jijni
Dar, na Alex nae akasema anatokea huko huko Dar yaani manzese. Ilikuwa zaidi ya
furaha kwa Rachael kusikia pia jamaa anatokea Dar na kwa haraka alipiga hesabu
kuwa ifikapo likizo watakuwa wote Dar.
Rachael akamwambia Alex kuwa siku
iliyofuata atatoka na hivyo ataenda likizo ya wiki moja ili akapumzike kwa Babu
yake hapo mahenge.
Ikumbukwe kuwa asili ya Rachael ni mpogoro wa
mahenge ingawa wazazi wake wapo DAR, ila huku ni kwa marehemu babu yake Mbunda
wa Mbunda. Hivyo alimwomba Alex kuwa pindi atakapotoka na kuchukua ruhusa ya
wiki waonane nyumbani kwa babu yake kwani ana mazungumzo na yeye hivyo aende
peke yake.
Alex alikubali lakini alimwomba wafanye keshokutwa kwani kesho
angekuwa bize sana na mambo ya shule na kuanzia saa nane mchana yaani baada ya
vipindi vya darasani anatakiwa aende benki kuchukua hela ya matumizi.
Rachael
kusikia hela ya matumizi akamwambia kwa hilo asiwe na hofu hiyo hela ya
matumizi ilipo banki aiache tu kwani yeye atampa zingine. Alex alishangaa sana
kusikia hivyo kwani hela alizotaka kwenda kuzichukua ni nyingi hivyo akamwambia
tena itanibidi niende tu kwani hela ninazotaka kuzichukua ni nyingi sana yaani
ni pamoja na ada ya shule. Lakini cha ajabu na kushangaza Rachael kwa kiburi na
dharau akamwambia hata ingekuwa ya nini bado angempa.
Hapa inanikumbusha nilipokuwa nikisoma mimi jirani
yetu kulikuwa na shule ya private wao walikuwa wakilipa milioni kwa mwaka alafu
sisi elfu sabini hivyo walikuwa wakitudharau sana wakidai ada yetu ni sawa
nahela yao ya matumizi kwa mwezi. Hapo Alex hakuwa na cha kujitetea tena zaidi
ya kukubali matokea na kutii ratiba ya Rachael.
Basi Alex aliporudi shuleni kwao akawapatia wenzie
stori ya yaliyori huko hospitalini, watu wakacheka na kufurahi sana na kila mtu
alijaribu kutoa ushauri wake, wapo waliosema ”kamatia hapo hapo mwanangu na
wengine walisema hafai kutokana na skendo zake kwanza usikute ana ukimwi
anausambaa kwa watu.” basi kila mtu alisema lake siunajua tena kwenye wengi
pana mengi lakini binafsi Alex aliamua kwenda kumsikiliza mrembo huyo.
Kesho ilifika na Alex alitimiza ahadi yake kwa
kufika kwa kina Rachael tena kwa mda waliokubaliana, alimkuta Rachael
akimsubiri kwa hamu na jam, akakaribishwa sebuleni na siku hiyo ndugu zake
Rachael hawakuwepo kwa mda huo bali kulikuwa na watoto wadogo ambao wasingeweza
kuathiri mazungumzo ya wawili huo.
Walizungumza mengi lakini kubwa na la muhimu
lilikuwa bado limefichwa. Kama kawaida yake binti huyu mwenye hulka za kizungu
alianza kutoa ya moyoni.
Alianza kwa kusema “Alex kuna kitu kimoja kinanisumbua
sana ndani ya uvungu wa moyo wangu, nmejitahidi kuvumilia lakini kila nikikuona
mwili wangu unakufa ganzi, nmeona nkwambie ukweli tu japo maadili ya kiafrika
hayaturuhusu kufanya hivyo. kiukweli ntapata nafuu kama utanirusu nisogee
karibu yako zaidi nkwambie ninachotaka kukuambia. ‘Alex alisita kidogo lakini
akamwambia wewe endelea tu nakusikilia..
Rachael akaendelea kusema 'mwenzio tangia
nilipokuona ile siku ya kwanza nilihisi mapigo ya moyo kwena mbio na baadhii ya
sehemu zangu kusisimuka ajabu, msisimko ulionipelekea kupata upweke wa ghafla,
ila kuna kitu kimoja kinachonifurahisha na kunifariji kutoka kwako na hii ni
mara baada ya kufanya uchunguzu wangu na kuwauliza rafiki zako kuhusu wewe
wakanieleza kuwa wewe ni mtu mzuri sana, mstaarabu, mpole na usiyependa shari
na kikubwa aidi wewe ni handsomeboy.
Kwa kweli umetokea kuuteka moyo wangu kwa
mda mfupi sana, nashindwa kujieleza zaidi kwani nahisi kurudiarudia maneno ila
ninachokuomba Alex mpenzi fungua moyo wako unipatie pumziko la milele kwani
nmechoshwa huko ntokako please.
ALEX naomba unielewe nakupenda sana, sauti hiyo
ilitoka kwa shida sana nahisia nzito ikiambatana na kwikwi zilizomsababishia
Alex kuwa kimya kama yupo kanisani alitamani akatishe maneno kwa kusema na yeye
anampenda lakini kukawa na sauti mbili inaopingana ndani ya moyo wake.
Alex baada ya kuona Rachael amekaa kimya na
kusubiri jibu aliamua kuvunja ukimya kwa kusema”kwa sasa sina jibu la kukupa
kwa sababu sikulitegemea hilo” Rachael hakuridhika ikabidi amuulize anachoogopa
ni nini ili hali yeye sio mtoto kama kuna kitu unaogopa niambie na mimi nikijue
au una girlfriend mwingine?. Alex akamwambia hapana ila nashindwa kuamini
msichana mzuri kama wewe usiwe na boyfriend au ndo unataka
kutuchanganya.
Rachael kwa sauti ya unyonge ”hapana my dear ila sijui
nikuelezaje mpaka unielewe,mimi niko mwenyewe nielewe mwana wa mwenzio
niepukane na hichi kilio, please nikubalie basi niondoke kwenye ulimwengu huu
wa upweke, safari hii Rachael alisimama na...........................................................
USIKOSE SEHEMU YA SITA